Maana ya neno afya na English translation

Maana ya neno afya

Matamshi: /afja/

Afya 1

(Nomino katika ngeli ya [i-zi])

Maana:

1. hali au siha njema ya mwili.

2. nguvu alizo nazo mtu.

Afya! 2

(Kihisishi)

Maana: tamko analotamka mtu kumtakia heri au uzima mtu mwingine akienda chafya.

Afya 3

(Kihisishi)

Maana: tamshi la watoto wanaposhawishiana kutenda jambo.

Afya Katika Kiingereza (English translation)

Afya katika Kiingereza ni: health, good health.

Related Posts