Maana ya neno agana na English translation

Posted by:

|

On:

|

Maana ya neno agana

Matamshi: /agana/

(Kitenzi si elekezi)

Maana:

1. ombeana heri.

2. afikiana na mtu kutenda jambo fulani.

Mnyambuliko wa agana: → agania, aganika, aganisha.

Agana Katika Kiingereza (English translation)

Agana katika Kiingereza inategemea maana unayokusudia:

Agana ya kuombeana heri ni: to say goodbye, to bid farewell (to each other)

Agana ya afikiana na mtu kutenda jambo fulani ni: agree, consent, or concur.