Maana ya neno ajabu
Matamshi: /ajabu/
Wingi wa ajabu ni maajabu.
Ajabu 1
(Nomino katika ngeli ya [li-ya])
Maana: jambo au kitu cha kushangaza. Visawe vyake ni: muujiza, kioja, shani.
Ajabu 2
(Kivumishi)
Maana: -iliyopita kiasi. Visawe vyake ni: mno, kupindukia, kiasi.
Mfano: Tatu ni mrembo ajabu.
Ajabu Katika Kiingereza (English translation)
Ajabu katika Kiingereza inategemea maana unayokusudia:
- Ajabu ya jambo au kitu cha kushangaza ni: a miracle, amazing, astonishing, strange, etc
- Ajabu ya -iliyopita kiasi ni: Extremely, very, incredibly, really, exceedingly, seriously, super, terrifically, awfully, awful, immensely, and hugely