Maana ya neno ajemi
Matamshi: /ajɛmi/
Ajemi 1
Maana: pia Uajemi, Iran.
Mfano: Zamani inasemekana mabaharia kutoka Ajemi walikuja pwani ya Afrika ya Mashariki.
Ajemi 2
(Nomino katika ngeli ya [i-zi)
Maana: mkate kama chapati uliookwa katika tanuri.
Ajemi Katika Kiingereza (English translation)
Ajemi katika Kiingereza inategemea maana unayokusudia:
- Ajemi ya uajemi ni: Iran ama Persian.
- Ajemi ya mkate wa chapati ni: round flat bread.