Maana ya neno akiba
Matamshi: /akiba/
Akiba 1
(Nomino katika ngeli ya [i-zi])
Maana: hifadhi inayowekwa kwa matumizi ya baadaye.
Mfano: Hamisi amejifungulia akaunti ya akiba kwa ajili ya siku za uzeeni.
Methali: Akiba haiozi: Unachokihifadhi leo kitakufaa kesho.
Akiba 2
(Nomino katika ngeli ya [i-zi])
Maana: programu kwenye tarakilishi ambayo ni hifadhi badala ya data.
Akiba Katika Kiingereza (English translation)
Akiba katika KIingereza inategemea na maana unayokusudia:
- Akiba (hifadhi inayowekwa kwa matumizi ya baadaye.) ni: Savings.
- Akiba (programu kwenye tarakilishi ambayo ni hifadhi badala ya data.) ni: Data backup program.