Maana ya neno akidi
Matamshi: /akidi/
Akidi 1
(Nomino katika ngeli ya [i-zi])
Maana: pia akdi, ufungaji harusi au ndoa. Kisawe chake ni nikaha.
Akidi 2
(Kitenzi elekezi)
Maana: timiza au fikia idadi inayostahili ili mkutano ufanyike.
Mfano: Mkutano hauwezi kufanyika iwapo hatutatimiza akidi.
Mnyambuliko wake ni: akidiana, akidika, akidisha, akidiwa.
Akidi 3
(Kitenzi elekezi)
Maana:
1. fanyia hila, danganya au ghushi.
2. hitimisha, kamilisha.
Mnyambuliko wake ni: akidia, akidiana, akidika, akidisha, akidiwa.
Akidi Katika Kiingereza (English translation)
Akidi katika KIingereza inategemea na maana unayokusudia:
- Akidi (ufungaji harusi au ndoa) ni: Marriage, wedding.
- Akidi (timiza au fikia idadi inayostahili ili mkutano ufanyike) ni: Reach the quorum for a meeting.
- Akidi (fanyia hila, danganya au ghushi) ni: Trick, deceive, forge.
- Akidi (hitimisha, kamilisha) ni: Finalize, complete.