Maana ya neno akifisha na English translation

Maana ya neno akifisha

Matamshi: /akifisha/

Akifisha 1

(Kitenzi elekezi)

Maana: weka alama fulani kwenye sentensi kama vile alama ya mshangao au alama ya kuuliza kuonyesha dhamira yake.

Mnyambuliko wake ni → akifishia, akifishiwa, akifishwa.

Akifisha 2

(Kitenzi elekezi)

Maana: zuia au kataza mtu asitende jambo fulani.

Mnyambuliko wake ni: → akifishana, akifishika, akifishikwa.

Akifisha Katika Kiingereza (English translation)

Akifisha katika KIingereza inategemea na maana unayokusudia:

  • Akifisha (weka alama fulani kwenye sentensi) ni: Punctuate, put punctuation marks.
  • Akifisha (zuia au kataza mtu asitende jambo fulani.) ni: Prevent, hinder, forbid.
Related Posts