Maana ya neno akifisha
Matamshi: /akifisha/
Akifisha 1
(Kitenzi elekezi)
Maana: weka alama fulani kwenye sentensi kama vile alama ya mshangao au alama ya kuuliza kuonyesha dhamira yake.
Mnyambuliko wake ni → akifishia, akifishiwa, akifishwa.
Akifisha 2
(Kitenzi elekezi)
Maana: zuia au kataza mtu asitende jambo fulani.
Mnyambuliko wake ni: → akifishana, akifishika, akifishikwa.
Akifisha Katika Kiingereza (English translation)
Akifisha katika KIingereza inategemea na maana unayokusudia:
- Akifisha (weka alama fulani kwenye sentensi) ni: Punctuate, put punctuation marks.
- Akifisha (zuia au kataza mtu asitende jambo fulani.) ni: Prevent, hinder, forbid.