Maana ya neno akika
Matamshi: /akika/
Akika 1
(Nomino katika ngeli ya [i-zi])
Maana: uchinjaji mbuzi au kondoo kulingana na mila na desturi ya jamii.
Akika 2
(Nomino katika ngeli ya [i-zi])
Maana: sherehe inayoambatana na mtoto mchanga kunyolewa nywele kwa mara ya kwanza.
Akika 3
(Nomino katika ngeli ya [i-zi])
Maana: bonde ambalo humomonyoka kutokana na majilio mengi ya maji ya mvua.
Akika Katika Kiingereza (English translation)
Akika katika KIingereza inategemea na maana unayokusudia:
- Akika (uchinjaji mbuzi au kondoo kulingana na mila) ni: Sacrificial slaughter of goat/sheep.
- Akika (sherehe inayoambatana na mtoto mchanga kunyolewa nywele kwa mara ya kwanza) ni: The first baby’s hair shaving ceremony
- Akika (: bonde ambalo humomonyoka kutokana na majilio mengi ya maji ya mvua) ni: Eroded valley.