Maana ya neno akili na English translation

Maana ya neno akili

Matamshi: /akili/

(Nomino katika ngeli ya [i-zi])

Maana:

1. utumiaji bongo katika kufanya maamuzi ya busara.

2. kipaji cha kufahamu na kujifunza maarifa ya dunia kwa jumla.

Methali: Akili nyingi huondoa maarifa: Usijifanye unafahamu kila kitu, huenda kitu kidogo kikakutia aibu au kukushinda.

Methali: Akili ni mali: Mtumia busara huchuma mali

Akili Katika Kiingereza (English translation)

Akili katika KIingereza inategemea na maana unayokusudia:

  • Akili (utumiaji bongo katika kufanya maamuzi ya busara) ni: Intelligence, wisdom.
  • Akili (kipaji cha kufahamu na kujifunza maarifa ya dunia kwa jumla) ni: Knowledge, ability to learn.
Related Posts