Maana ya neno akili
Matamshi: /akili/
(Nomino katika ngeli ya [i-zi])
Maana:
1. utumiaji bongo katika kufanya maamuzi ya busara.
2. kipaji cha kufahamu na kujifunza maarifa ya dunia kwa jumla.
Methali: Akili nyingi huondoa maarifa: Usijifanye unafahamu kila kitu, huenda kitu kidogo kikakutia aibu au kukushinda.
Methali: Akili ni mali: Mtumia busara huchuma mali
Akili Katika Kiingereza (English translation)
Akili katika KIingereza inategemea na maana unayokusudia:
- Akili (utumiaji bongo katika kufanya maamuzi ya busara) ni: Intelligence, wisdom.
- Akili (kipaji cha kufahamu na kujifunza maarifa ya dunia kwa jumla) ni: Knowledge, ability to learn.