Maana ya neno akisi
Matamshi /akisi/
Akisi 1
(Kitenzi elekezi)
Maana: dunda kwa miale au mionzi ya mwanga mahali kama vile uso wa kioo au sura ya maji baharini, mtoni na ziwani.
(Mfano): Kioo changu kimezeeka; hakiakisi tena vizuri.
Mnyambuliko wake ni: → akisia, akisiana, akisika, akisisha, akisiwa.
Akisi 2
(Kitenzi elekezi)
Maana: toa ishara ya jambo fulani.
Mnyambuliko wake ni : → akisia, akisiana, akisika, akisisha, akisiwa.
Akisi 3
(Kitenzi elekezi)
Maana: lipa deni polepole katika muda mwafaka.
Akisi Katika Kiingereza (English translation)
Akisi katika KIingereza inategemea na maana unayokusudia:
- Akisi (dunda kwa miale au mionzi ya mwanga mahali kama vile uso wa kioo au sura ya maji) ni: Reflection.
- Akisi (toa ishara ya jambo fulani) ni: to show.
- Akisi (lipa deni polepole katika muda mwafaka) ni: to pay off a debt in installments.