Maana ya neno akrabu
Matamshi: /akrabu/
Akrabu 1
(Nomno katika ngeli ya [i-zi])
Maana: pia akraba,
1. mshale au mkono wa saa.
2. mshale au mkono wa mizani.
3. mwelekeo mmoja wa pande za dira.
Akrabu 2
(Nomino katika ngeli ya [i-zi])
Maana: pia akraba, alama ya nge katika mfumo wa nyota angani.
Akrabu Katika Kiingereza (English translation)
Akrabu katika KIingereza inategemea na maana unayokusudia:
- Akrabu (mshale au mkono wa saa) ni: hand of a clock.
- Akrabu (mshale au mkono wa mizani) ni: pointer, hand of a scale.
- Akrabu (mwelekeo mmoja wa pande za dira) ni: cardinal direction.
- Akrabu (alama ya nge katika mfumo wa nyota angani) ni: Scorpio or scorpius (constellation).