Maana ya neno ala
Matamshi: /ala/
Ala 1
(Nomino katika ngeli ya [i-zi])
Maana: kifuko kinachopachikwa kiunoni cha kuchomekea kisu, jambia au upanga.
Mfano: Ala ya jambia lake imezeeka mno.
Methali: Ala moja haikai panga mbili: Watu wawili wanaogombea kitu kimoja hawawezi kusikilizana.
Ala 2
(Nomino katika ngeli ya [i-zi])
Maana: zana ya kutendea kazi kama vile uundaji wa kitu, uporomoshaji wa muziki.
Ala! 3
(Kihisishi)
Maana: tamko linalofichua hisia za kushangaa au kushtuka.
Ala Katika Kiingereza (English translation)
Ala katika Kiingereza inategemea maana unayokusudia:
- Ala (kifuko kinachopachikwa kiunoni cha kuchomekea kisu, jambia au upanga) ni: sheath for a knife or dagger.
- Ala (zana ya kutendea kazi) ni: tool, instrument.
- Ala! (tamko linalofichua hisia za kushangaa au kushtuka) ni: exclamation of suprise like: Eep! Golly! Ha! Huh! Whoa! Wow! Yikes!