Maana ya neno alama
Matamshi: /alama/
Alama1
(Nomino katika ngeli ya [i-zi])
Maana: doa linalochafua kitu kama vile nguo, meza n.k.
Alama 2
(Nomino katika ngeli ya [i-zi])
1. maksi anazopewa mtu baada ya kufanya mtihani au katika shindano.
2. kitambulisho kama vile cha maandishi elekezi barabarani au umbo la nyayo za wanyama msituni.
Alama 3
(Nomino katika ngeli ya [i-zi])
Maana: ishara ya uakifishaji.
Alama Katika Kiingereza (English translation)
Alama katika Kiingereza inategemea na maana unayokusudia:
- Alama (linalochafua kitu) ni: stain, mark.
- Alama (maksi anazopewa mtu) ni: grade, score, marks.
- Alama (ishara ya uakifishaji) ni: punctuation mark.