Maana ya neno alika na English translation

Maana ya neno alika

Matamshi:  /alika/

Alika 1

(Kitenzi elekezi)

1. karibisha mtu ahudhurie shughuli au sherehe.

2. tangaza au nadi.

Mnyambuliko wa ke ni: → alikana, alikia, alikika, alikiwa, alikwa.

Alika 2

(Kitenzi si elekezi)

Maana: mlio wa kufyatuka risasi.

Mnyambuliko  wake ni: → alikia, alikika; alikisha.

Alika 3

(Kitenzi elekezi)

Maana: pia alisa,

1. weka mgonjwa mahali kwa ajili ya tiba.

2. tawisha mwari kwa siku fulani kabla ya siku ya harusi yake.

Alika 4

(Nomino katika ngeli ya [a-wa])

Maana: pia arika, kijana aliyefunzwa jandoni au unyagoni.

Alika Katika Kiingereza (English translation)

Alika katika Kiingereza inategemea na maana unayokusudia:

  • Alika (karibisha mtu ahudhurie shughuli au sherehe) ni: invite.
  • Alika (tangaza au nadi) ni: announce.
  • Alika (mlio wa kufyatuka risasi) ni: gunshot.
  • Alika (weka mgonjwa mahali kwa ajili ya tiba) ni: hospitalize, quarantine.
  • Alika (tawisha mwari kwa siku fulani kabla ya siku ya harusi yake) ni: keeping the bride and groom separate until wedding day.
  • Alika (kijana aliyefunzwa jandoni au unyagoni) ni: warrior – a young man trained after circumcision.
Related Posts