Maana ya neno amba
Matamshi: /amba/
Amba 1
(Kitenzi elekezi)
1. zungumza au sema.
Mfano: Kaka waambaje?
2. sengenya.
Mnyambuliko wake ni: → ambana, ambania, ambanika, ambanisha, ambiwa.
Amba 2
(Kielezi)
Maana: labda, huenda, asaa, pengine.
Amba! 3
(Kihisishi)
Maana: tamko linalotolewa kama kubalio la jambo. Visawe vyake ni: naam, hasa, barabara.
Amba- 4
(Kivumishi)
Maana: kirejeshi cha kutoa sifa za nomino au kiwakilishi chake kifungamanishwacho na “o” rejeshi.
Amba Katika Kiingereza (English translation)
Amba katika Kiingereza inategemea na maana unayokusudia:
- Amba (zungumza au sema) ni: speak.
- Amba (sengenya) ni: gossip.
- Amba (tamko linalotolewa kama kubalio la jambo) ni: maybe, perhaps.
- Amba-(Kivumishi kirejeshi) ni: demonstrative pronoun who.