Maana ya neno ambika na English translation

Posted by:

|

On:

|

Maana ya neno ambika

Matamshi: /ambika/

Ambika 1

(Kitenzi elekezi)

Maana:

1. andaa mtego wa samaki kwa nyavu katika maji yenye kina kirefu au maji mafu.

2. tega chambo katika mshipi wa uvuvi.

3. loweka au didimiza majini.

Mnyambuliko wake ni: → ambikia, ambikiana, ambikisha, ambikwa.

Ambika 2

(Kitenzi elekezi )

Maana: zulia au singizia mtu uwongo au habari zisizo kweli.

Mnyambuliko wake ni: Ambikana, ambikia, ambikika, ambikisha, ambikiwa.

Ambika Katika Kiingereza (English translation)

Ambika katika Kiingereza inategemea na maana unayokusudia:

  • Ambika (andaa mtego wa samaki kwa nyavu katika maji yenye kina kirefu au maji mafu) ni: setting up a fish trap.
  • Ambika (tega chambo katika mshipi wa uvuvi) ni: to put a bait on a fishing line.
  • Ambika (loweka au didimiza majini) ni: To soak or dip in water, immersing, submerging.
  • Ambika (zulia au singizia mtu uwongo au habari zisizo kweli) ni: “slander” or “defamation.” (Making false statements against someone)