Maana ya neno ambisha
Matamshi: /ambisha/
(Kitenzi elekezi)
Maana:
1. pia ambisa, sogeza na kupanga vitu kwa mkaribiano kama vile kuziweka dau, ngalawa au mashua pamoja ufukweni; funganisha chombo kimoja cha bahari na chombo kingine.
2. ongeza silabi kisarufi kwenye mzizi wa neno.
Mnyambuliko wake ni → ambishia, ambishiana, ambishika, ambishwa.
Ambisha Katika Kiingereza (English translation)
Ambisha katika Kiingereza ni:
- Ambisha (sogeza na kupanga vitu kwa mkaribiano) ni: move and arrange things close together.
- Ambisha (ongeza silabi kisarufi kwenye mzizi wa neno) ni: affixation.