Maana ya neno ambisha na English translation

Maana ya neno ambisha

Matamshi: /ambisha/

(Kitenzi elekezi)

Maana:

1. pia ambisa, sogeza na kupanga vitu kwa mkaribiano kama vile kuziweka dau, ngalawa au mashua pamoja ufukweni; funganisha chombo kimoja cha bahari na chombo kingine.

2. ongeza silabi kisarufi kwenye mzizi wa neno.

Mnyambuliko wake ni → ambishia, ambishiana, ambishika, ambishwa.

Ambisha Katika Kiingereza (English translation)

Ambisha katika Kiingereza ni:

  • Ambisha (sogeza na kupanga vitu kwa mkaribiano) ni: move and arrange things close together.
  • Ambisha (ongeza silabi kisarufi kwenye mzizi wa neno) ni: affixation.
Related Posts