Maana ya neno amili na English translation

Posted by:

|

On:

|

Maana ya neno amili

Matamshi: /amili/

Amili 1

(Kitenzi elekezi)

Maana: jua, fahamu, maizi, tambua, ng’amua, elewa.

Mnyambuliko wake ni: →amilia, amiliana, amilika, amilisha, amiliwa.

Amili 2

(Kitenzi elekezi)

1. tenda kazi au shughuli. Kisawe chake ni shughulika.

2. unda au tengeneza.

3. karabati au rekebisha kitu kilichoharibika.

Mnyambuliko wake ni: → amilia, amiliana, amilika, amilisha, amiliwa.

Amili Katika Kiingereza (English translation)

Amili katika Kiingereza inategemea na maana unayokusudia:

  • Amili (jua, fahamu, maizi, tambua, ng’amua, elewa) ni: know, realize, decide, understand.
  • Amili (tenda kazi au shughuli) ni: work.
  • Amili (unda au tengeneza) ni: create.
  • Amili (karabati au rekebisha kitu kilichoharibika) ni: repair.