Maana ya neno amini
Matamshi: /amini/
Amini 1
(Kitenzi elekezi)
Maana:
1. sadiki au kubalia ukweli wa kitu au jambo.
2. kubali kuwa fulani anakubalika.
Mfano: Juma hakuniangusha tamashani ndiyo maana ninamuamini.
Mnyambuliko wa amini ni: → aminia, aminiana, aminika, aminisha, aminiwa.
Amini 2
(Kitenzi elekezi)
Maana: sadiki na tekeleza mafunzo ya dini.
Mfano: Dini kuu duniani zinaamini kuwa Mungu ni mmoja.
Mnyambuliko wake ni: → aminia, aminiana, aminika, aminisha, aminiwa.
Amini Katika Kiingereza (English translation)
Amini katika Kiingereza inategemea na maana unayokusudia:
- Amini (sadiki au kubalia ukweli wa kitu au jambo) ni: believe or accept the truth of something.
- Amini (kubali kuwa fulani anakubalika) ni: trust.
- Amini (sadiki na tekeleza mafunzo ya dini) ni: faith or religious adherence.