Maana ya neno aminisha na English translation

Maana ya neno aminisha

Matamshi: /aminisha/

(Kitenzi elekezi)

Maana:

1. acha kitu au jambo chini ya mamlaka ya mtu.

2. thubutu au jasiri kufanya jambo la hatari.

3. sadikisha mtu juu ya kitu au jambo fulani.

Mnyambuliko wake ni: → aminishana, aminishia, aminishika, aminishwa.

Aminisha Katika Kiingereza (English translation)

Aminisha katika Kiingereza inategemea na maana unayokusudia:

  • Aminisha (acha kitu au jambo chini ya mamlaka ya mtu) ni: entrust.
  • Aminisha (thubutu au jasiri kufanya jambo la hatari) ni: empower, make someone brave.
  • Aminisha (sadikisha mtu juu ya kitu au jambo fulani) ni: assure.
Related Posts