Maana ya neno amka na English translation

Maana ya neno amka

Matamshi: /amka/

(Kitenzi si elekezi)

Maana:

1. toka kitandani au usingizini; fumbua macho.

Mfano: Babake Juma amechelewa kwenda uvuvini kwa sababu hakuamka alfajiri.

2. janjaruka, zinduka, changamka au erevuka.

3. simama wima au inuka.

Mfano: Mgeni wa heshima alipoingia ukumbini, watu wote waliaka na kusimama.

Mnyambuliko wake ni: → amkia, amkika, amkisha, amkiwa.

Amka Katika Kiingereza (English translation)

Amka katika Kiingereza inategemea na maana unayokusudia:

  • Amka (toka kitandani au usingizini; fumbua macho) ni: wake up, arise.
  • Amka (janjaruka, zinduka, changamka au erevuka) ni: become active, wise.
  • Amka (simama wima au inuka) ni: stand up, arise.
Related Posts