Maana ya neno amkia na English translation

Posted by:

|

On:

|

Maana ya neno amkia

Matamshi: /amkia/

Amkia 1

(Kitenzi elekezi)

Maana: amkua, sabahi, salimu mtu; julia mtu hali.

Mfano: Juma huwaamkia wazazi wake kila asubuhi.

Mnyambuliko wake ni: → amkiana, amkika, amkilia, amkisha, amkiwa.

Amkia 2

(Kitenzi si elekezi)

Maana: mkesha wa; tangulia siku fulani.

Mfano: Mwezi umeandama kwa hiyo kesho tutaamkia Sikuu ya Idd.

Amkia Katika Kiingereza  (English translation)

Amkia katika Kiingereza inategemea na maana unayokusudia:

  • Amkia (amkua, sabahi, salimu mtu; julia mtu hali) ni: greet, accost, salute.
  • Amkia (mkesha wa; tangulia siku fulani) ni: the eve of; a day that precedes a certain day.