Maana ya neno amsha na English translation

Posted by:

|

On:

|

Maana ya neno amsha

Matamshi: /amsha/

(Kitenzi elekezi)

Maana:

1. fanya mtu ashtuke na kufumbua macho kutoka usingizini.

2. zindusha au erevusha juu ya kitu au jambo.

Methali: Ukimwamsha aliyelala, utalala wewe: Usifunue siri ya kufanikisha mambo kwa mtu fulani ama sivyo atakuja kukuzidi au kukupita.

Mnyambuliko wake ni: → amshana, amshia, amshika, amshwa.

Amsha Katika Kiingereza (English translation)

Amsha katika Kiingereza inategemea na maana unayokusudia:

  • Amsha (fanya mtu ashtuke na kufumbua macho kutoka usingizini) ni: To wake up, arouse.
  • Amsha (zindusha au erevusha juu ya kitu au jambo) ni: enkindle, rouse, stimulate activate.