Sajili ni nini?
Sajili ni matumizi ya lugha katka mazingiza mbalimbali, inayoifanya lugha kubadilibadlika.
Aina za sajili na sifa zake
Sifa za sajili ya sokoni
- Ni lugha ambayo imejaa maswali. Kwa mfano: Mteja: Muuzaji, hii ngapi? Muuzaji: Mia Moja ishirini, Wewe una ngapi?
- Huchanganya lugha, mfano muuzaji husema bei ni ten, ten. Kumi, kumi
- Matumizi ya lugha kali haswa kwa wateja wasiokuwa na uvumilivu mfano: Fanya haraka ama niende zangu.
- Huwa na misamiati maalum kama vile ‘customer’, ‘karibia, karibia’, ’bei ni ya kurusha’, ‘mali ni fresh kabisa’, ‘bei ni ya chioni’, na menginevyo.
- Hutumia lugha ya ushawishi, kama vile; tafadhali.
- Wauzaji hutumia sauti ya juu ili kuwavutia wateja.
- Lugha hazingatii kanuni za sarufi.
- Hutumia lugha ya mkato.
- Lugha hujaa porojo.
Sifa za sajili ya mahakama
- Misamiati maalumu hutumika, kama vile mshukiwa, katiba, sheria, mashtaka, hakimu, Ushahidi, wakili, jela.
- Huwa na maelezo marefu na ya kina ili kutafuta ushahidi wowote uliopo.
- Ni lugha yenye kunukuu sana hasa vipengele katika vitabu vya sheria kama vile katiba.
- Ni lugha rasmi na sanifu.
- Ni lugha iliyojaa maswali na majibizano.
- Ni lugha yenye heshima.
Sifa za sajili ya michezo
- Matumizi ya ishara, kama vile kuinua mkono, kuonyesha kuumia uwanjani
- Sentensi huwa fupi fupi kama vile stars ya lazwa.
- Lugha si sanifu
- Kuna matumizi ya msamiati maalum, kama vile kandanda
Sifa za sajili ya shuleni
- Imesheheni lugha na msamiati inayoshikamana na mazingara ya elimu
- Utumizi wa lugha sanifu hutumika kwa wingi.
- Aghalabu shughuli hufuata utaratibu wa ratiba
- Inatumia maswali na majibu
Sifa za sajili ya hospitalini
- Matumizi ya lugha ya mahojiano
- Hutumia lugha ya upole
- Hutumia msamiati za hospitali k.m vile dawa , sindano au mgonjwa
- Hutumia lugha mwafaka na sanifu
- Kuna kuchanganya ndimi na kubadili msimbo
- Kuna matumizi ya maswali na majibu
Sifa za sajili ya vijana
- Kuna kuchanganya ndimi
- Ufupisho wa maneno k.m “wewe”huandikwa “ww”
- Hutumia lugha ya sheng
- Lugha hubadilikabadilika kulingana na mazingira
- Hutumia chuku
Sifa za sajili ya polisi
- Kuna kuchanganya ndimi
- Hutumia lugha yenye ukali
- Matumizi ya sentensi refu refu
- Hutumia lugha yenye maswali
- Hutumia lugha yenye vitisho