Maana ya sajili

Posted by:

|

On:

|

Sajili ni nini?

Sajili ni matumizi ya lugha katka mazingiza mbalimbali, inayoifanya lugha kubadilibadlika.

Aina za sajili na sifa zake

Sifa za sajili ya sokoni

 • Ni lugha ambayo imejaa maswali. Kwa mfano: Mteja: Muuzaji, hii ngapi? Muuzaji: Mia Moja ishirini, Wewe una ngapi?
 • Huchanganya lugha, mfano muuzaji husema bei ni ten, ten. Kumi, kumi
 • Matumizi ya lugha kali haswa kwa wateja wasiokuwa na uvumilivu mfano: Fanya haraka ama niende zangu.
 • Huwa na misamiati maalum kama vile ‘customer’, ‘karibia, karibia’, ’bei ni ya kurusha’, ‘mali ni fresh kabisa’, ‘bei ni ya chioni’, na menginevyo.
 • Hutumia lugha ya ushawishi, kama vile; tafadhali.
 • Wauzaji hutumia sauti ya juu ili kuwavutia wateja.
 • Lugha hazingatii kanuni za sarufi.
 • Hutumia lugha ya mkato.
 • Lugha hujaa porojo.

Sifa za sajili ya mahakama

 • Misamiati maalumu hutumika, kama vile mshukiwa, katiba, sheria, mashtaka, hakimu, Ushahidi, wakili, jela.
 • Huwa na maelezo marefu na ya kina ili kutafuta ushahidi wowote uliopo.
 • Ni lugha yenye kunukuu sana hasa vipengele katika vitabu vya sheria kama vile katiba.
 • Ni lugha rasmi na sanifu.
 • Ni lugha iliyojaa maswali na majibizano.
 • Ni lugha yenye heshima.

Sifa za sajili ya michezo

 • Matumizi ya ishara, kama vile kuinua mkono, kuonyesha kuumia uwanjani
 • Sentensi huwa fupi fupi kama vile stars ya lazwa.
 • Lugha si sanifu
 • Kuna matumizi ya msamiati maalum, kama vile kandanda

Sifa za sajili ya shuleni

 • Imesheheni lugha na msamiati inayoshikamana na mazingara ya elimu
 • Utumizi wa lugha sanifu hutumika kwa wingi.
 • Aghalabu shughuli hufuata utaratibu wa ratiba
 • Inatumia maswali na majibu

Sifa za sajili ya hospitalini

 • Matumizi ya lugha ya mahojiano
 • Hutumia lugha ya upole
 • Hutumia msamiati za hospitali k.m vile dawa , sindano au mgonjwa
 • Hutumia lugha mwafaka na sanifu
 • Kuna kuchanganya ndimi na kubadili msimbo
 • Kuna matumizi ya maswali na majibu

Sifa za sajili ya vijana

 • Kuna kuchanganya ndimi
 • Ufupisho wa maneno k.m “wewe”huandikwa “ww”
 • Hutumia lugha ya sheng
 • Lugha hubadilikabadilika kulingana na mazingira
 • Hutumia chuku

Sifa za sajili ya polisi

 • Kuna kuchanganya ndimi
 • Hutumia lugha yenye ukali
 • Matumizi ya sentensi refu refu
 • Hutumia lugha yenye maswali
 • Hutumia lugha yenye vitisho