Hapa kuna methali 50 zinazozungumzia kufanya kazi kwa bidii. Kutokana na hizi methali utapata motisha ya kufanya kazi kwa bidii ili ufanikiwe.
Methali za bidii
- Ajizi ni nyumba ya njaa
Methali hii inamaanisha uvivu unafanya mtu kuishi kwa umaskini.
- Aisyekubali kushindwa si mshindani
Methali hii inamaanisha kwamba katika maisha kuna kupata na kukosa.
- Atangaye na jua hujua
Methali hii inamaanisha kwamba anayejibidiisha na kutafuta hupata.
- Baada ya dhiki faraja
Methali hii inamaanisha kwamba baada ya mateso utapata furaha.
- Bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi
Methali hii ina maana kwamba kila mtu ana bahati yake.
- Bandu bandu humaliza gogo
Methali hii inamaanisha kwamba kufanya kitu kidogo kidogo hatimaye humaliza kazi kubwa.
- Bura yangu sibadili kwa Rehani
Methali hii ina maana kwamba usitupe kitu chako, hata kama ni kibaya, ukitamani cha mwenzio.
- Chanda chema huvikwa pete
Methali hii ina maana kwamba anayefanya mema atatuzwa.
- Chelewa chelewa, utakuta mwana si wako
Methali hii inamaanisha kwamba anayekuwa wa kwanza, hupata mambo mazuri.
- Chovya chovya humaliza buyu laa asali
Methali hii ina maana kwamba kufanya jambo kidogokidogo, humaliza jambo zima.
- Chungu kidogo huchemka upesi
Methali hii ina maana kwamba heri kufanya mambo madogo kwa haraka, kuliko mambo mengi kwa muda mrefu.
- Chururu si ndondo
Methali hii ina maana kwamba heri kupata vitu vidogo vya kudumu kuliko vingi mara moja.
- Debe shinda haliachi kutika
Methali hii inamaanisha kuwa wengi sana hupenda kusema bila kuonyesha utendaji.
- Kazi mbi si mchezo mwema
Methali hii ina maana kwamba Kazi ngumu haina raha.
- Kulea mimba si kazi kazi kulea mwana
Methali hii ina maana kwmaba kulea mtoto ni kazi ngumu kuliko kubeba mimba.
- Kuvua si kazi kazi ni magawioni
Methali hii ina maana kwamba kazi halisi ni kupata samaki, sio kuvua.
- Mume ni kazi mke ni nguo
Kazi hii ina maana kwamba mume ni jukumu, mke ni raha.
- Mzoea udalali hawezi kazi ya duka
Methali hii ina maana kwamba mtu aliyezoea kazi moja hawezi kufanya kazi nyingine kirahisi.
- Eda ni ada yenye faida
Methali hii ina maana kwamba uvumilivu na busara mara nyingi humnufaisha mwanadamu.
- Fahari isiyo na ari haina heri
Methali hii ina maana kwamba utukufu hauwezi kuja bila kufanya kazi.
- Fimbo ya mbali haiui nyoka
Methali hii ina maana kwamba kitu kilicho mbali hakiwezi kukupa msaada wa haraka.
- Haba na haba hujaza kibaba.
Methali hii ina maana kwamba usidharau mambo madogo madogo kwa kuwa hayo ndiyo huishia kuwa makubwa baadaye.
- Hakuna ziada mbovu
Methali hii inamaanisha kuwa chochote mtu apatacho chafaa.
- Hatua moja hufupisha safari.
Methali hii inamaanisha kwamba hatua moja anayopiga binadamu anapotembea husaidia kufupisha mwendo.
- Heri kwaa ya dole kuliko kwaa ya ulimi
Methali hii ina maana kwamba afadhali kukosea katika kutembea ukaumia kuliko kutamka maneno yatakayosababisha mgogoro.
- Debe tupu haliachi kuvuma
Methali hii ina maana kwamba hata kitu kisicho na thamani kinazungumziwa sana.
- Heri nusu shari kuliko shari kamili
Methali hii ina maana kwamba ni bora kupata matokeo mabaya kidogo kutopata hata kitu.
- Subira yavuta heri na huleta kilicho mbali
Methali hii ina maana kwamba subira huleta matokeo mazuri.
- Heri kujikwaa kidole kuliko ulimi
Hii methali inamaanisha kuwa ni bora kufanya makosa madogo kuliko makubwa.
- Kila ndege huruka kwa ubawa wake
Methali hii ina maana kwamba kila mtu hufanya kazi au kufanya shughuli zake kulingana na uwezo wake.
- Kitegwacho kukitega kwataka ubongo
Methali hii ina maana kwamba kazi yoyote inahitaji akili na ujuzi ili kuitekeleza.
- Kula kutamu kulima mavune
Methali hii ina maana kwamba watu hupenda kufaidi bila kujihangaisha.
- Kula uhondo kwataka matendo
Methali hii inamaanisha kuwa ili tuwe na maisha mema sharti tufanye kazi kwa bidi.
- Kuzima koleo si mwisho wa uhunzi
Methali hii ina maana kwamba kupumzika siyo kuacha kazi.
- Kwa mwoga huenda kicheko, kwa shujaa huenda kilio
Methali hii ina maana kuwa usipambane na jambo usiloliweza.
- Maisha ni bahati ifumbate
Methali hii inamaanisha kuwa uhai ni majaaliwa utumie vizuri, maisha ni vita pigana ili uishi ni sharti uhangaike.
- Mali bila daftari hupotea bila habari
Methali hii inamaanisha utunzaji wa kitu kwa umakini unahitaji uwekaji mzuri wa kumbukumbu.
- Mbio za sakafuni huishia ukingoni
Methali hii inamaanisha jambo lenye mwanzo lazima liwe na mwisho, kwenda mbio sio kufika, kufanya jambo kwa haraka kunaweza kusiwe na matokeo mazuri.
- Mchagua jembe si mkulima
Methali hii ina maana kuwa mwenye nia ya dhati hachagui kitendea kazi mtu mvivu husingizia vitendea kazi.
- Mchele mmoja mapishi mbalimbali
Methali hii ina maana kuwa jambo moja linaweza kufanywa kwa namna mbalimbali.
- Mchelea bahari si msafiri
Methali hii ina maana kuwa anayeiogopa bahari, hawezi kusafiri majini.
- Mcheza hawi kiwete ngoma yataka matao
Methali hii ina maana kuwa kila shughuli anayoifanya binadamu inapaswa kufanywa kwa bidii na kujituma kwingi.
- Mfa maji haishi kutapatapa
Methali hii ina maana kuwa mtu akipatwa na shida hutumia njia yoyote ili kujinusuru.
- Mgaagaa na upwa, hali wali mkavu
Methali hii ina maana kuwa anayepita mahali penye riziki mara kwa mara aweza kubahatika.
- Mkono mtupu haulambwi
Methali hii inamaanisha kuwa kama hauna kitu hutasaidika, lazima toa kitu ili upate kitu.
- Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni
Hii methali ni kama mnyonge hana haki mpaka mwenye nguvu apende.
- Mstahimilivu hula mbivu
Methali hii ina maana kuwa uvumilivu hadi mwisho unahitajika katika kufikia mema.
- Mtaka cha mvunguni sharti ainame
Methali hii ina maana kuwa ili kupata mafanikio lazima kupitia misukosuko.
- Mvumilivu hula mbivu
Methali hii ina maana kuwa mtu anayevumilia taabu na shida nyingi hupata mafaniko maishani.
- Mwenda pole hajikwai
Methali hii ina maana kuwa ukifanya jambo kwa utaratibu utafanikiwa.
- Mwenye nguvu mpishe
Methali hii ina maana kuwa si busara kupambana na mtu anayekuzidi uwezo.
- Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu
Methali hii ina maana kuwa ni vizuri kushirikiana na binadamu wenzio.
- Kula ni vyepesi lakini kulima ng’o
Methali ina maana kuwa kupata chakula ni rahisi kuliko kufanya kazi ili kupata chakula hicho.
One response to “Methali 50 za bidii”