Methali 50 za bidii

Posted by:

|

On:

|

Hapa kuna methali 50 zinazozungumzia kufanya kazi kwa bidii. Kutokana na hizi methali utapata motisha ya kufanya kazi kwa bidii ili ufanikiwe.

Methali za bidii

 • Ajizi ni nyumba ya njaa

Methali hii inamaanisha uvivu unafanya mtu kuishi kwa umaskini.

 • Aisyekubali kushindwa si mshindani

Methali hii inamaanisha kwamba katika maisha kuna kupata na kukosa.

 • Atangaye na jua hujua

Methali hii inamaanisha kwamba anayejibidiisha na kutafuta hupata.

 • Baada ya dhiki faraja

Methali hii inamaanisha kwamba baada ya mateso utapata furaha.

 • Bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi

Methali hii ina maana kwamba kila mtu ana bahati yake.

 • Bandu bandu humaliza gogo

Methali hii inamaanisha kwamba kufanya kitu kidogo kidogo hatimaye humaliza kazi kubwa.

 • Bura yangu sibadili kwa Rehani

Methali hii ina maana kwamba usitupe kitu chako, hata kama ni kibaya, ukitamani cha mwenzio.

 • Chanda chema huvikwa pete

Methali hii ina maana kwamba anayefanya mema atatuzwa.

 • Chelewa chelewa, utakuta mwana si wako

Methali hii inamaanisha kwamba anayekuwa wa kwanza, hupata mambo mazuri.

 • Chovya chovya humaliza buyu laa asali

Methali hii ina maana kwamba kufanya jambo kidogokidogo, humaliza jambo zima.

 • Chungu kidogo huchemka upesi

Methali hii ina maana kwamba heri kufanya mambo madogo kwa haraka, kuliko mambo mengi kwa muda mrefu.

 • Chururu si ndondo

Methali hii ina maana kwamba heri kupata vitu vidogo vya kudumu kuliko vingi mara moja.

 • Debe shinda haliachi kutika

Methali hii inamaanisha kuwa wengi sana hupenda kusema bila kuonyesha utendaji.

 • Kazi mbi si mchezo mwema

Methali hii ina maana kwamba Kazi ngumu haina raha.

 • Kulea mimba si kazi kazi kulea mwana

Methali hii ina maana kwmaba kulea mtoto ni kazi ngumu kuliko kubeba mimba.

 • Kuvua si kazi kazi ni magawioni

Methali hii ina maana kwamba kazi halisi ni kupata samaki, sio kuvua.

 • Mume ni kazi mke ni nguo

Kazi hii ina maana kwamba mume ni jukumu, mke ni raha.

 • Mzoea udalali hawezi kazi ya duka

Methali hii ina maana kwamba mtu aliyezoea kazi moja hawezi kufanya kazi nyingine kirahisi.

 • Eda ni ada yenye faida

Methali hii ina maana kwamba uvumilivu na busara mara nyingi humnufaisha mwanadamu.

 • Fahari isiyo na ari haina heri

Methali hii ina maana kwamba utukufu hauwezi kuja bila kufanya kazi.

 • Fimbo ya mbali haiui nyoka

Methali hii ina maana kwamba kitu kilicho mbali hakiwezi kukupa msaada wa haraka.

 • Haba na haba hujaza kibaba.

Methali hii ina maana kwamba usidharau mambo madogo madogo kwa kuwa hayo ndiyo huishia kuwa makubwa baadaye.

 • Hakuna ziada mbovu

Methali hii inamaanisha kuwa chochote mtu apatacho chafaa.

 • Hatua moja hufupisha safari.

Methali hii inamaanisha kwamba hatua moja anayopiga binadamu anapotembea husaidia kufupisha mwendo.

 • Heri kwaa ya dole kuliko kwaa ya ulimi

Methali hii ina maana kwamba afadhali kukosea katika kutembea ukaumia kuliko kutamka maneno yatakayosababisha mgogoro.

 • Debe tupu haliachi kuvuma

Methali hii ina maana kwamba hata kitu kisicho na thamani kinazungumziwa sana.

 • Heri nusu shari kuliko shari kamili

Methali hii ina maana kwamba ni bora kupata matokeo mabaya kidogo kutopata hata kitu.

 • Subira yavuta heri na huleta kilicho mbali

Methali hii ina maana kwamba subira huleta matokeo mazuri.

 • Heri kujikwaa kidole kuliko ulimi

Hii methali inamaanisha kuwa ni bora kufanya makosa madogo kuliko makubwa.

 • Kila ndege huruka kwa ubawa wake

Methali hii ina maana kwamba kila mtu hufanya kazi au kufanya shughuli zake kulingana na uwezo wake.

 • Kitegwacho kukitega kwataka ubongo

Methali hii ina maana kwamba kazi yoyote inahitaji akili na ujuzi ili kuitekeleza.

 • Kula kutamu kulima mavune

Methali hii ina maana kwamba watu hupenda kufaidi bila kujihangaisha.

 • Kula uhondo kwataka matendo

Methali hii inamaanisha kuwa ili tuwe na maisha mema sharti tufanye kazi kwa bidi.

 • Kuzima koleo si mwisho wa uhunzi

Methali hii ina maana kwamba kupumzika siyo kuacha kazi.

 • Kwa mwoga huenda kicheko, kwa shujaa huenda kilio

Methali hii ina maana kuwa usipambane na jambo usiloliweza.

 • Maisha ni bahati ifumbate

Methali hii inamaanisha kuwa uhai ni majaaliwa utumie vizuri, maisha ni vita pigana ili uishi ni sharti uhangaike.

 • Mali bila daftari hupotea bila habari

Methali hii inamaanisha utunzaji wa kitu kwa umakini unahitaji uwekaji mzuri wa kumbukumbu.

 • Mbio za sakafuni huishia ukingoni

Methali hii inamaanisha jambo lenye mwanzo lazima liwe na mwisho, kwenda mbio sio kufika, kufanya jambo kwa haraka kunaweza kusiwe na matokeo mazuri.

 • Mchagua jembe si mkulima

Methali hii ina maana kuwa mwenye nia ya dhati hachagui kitendea kazi mtu mvivu husingizia vitendea kazi.

 • Mchele mmoja mapishi mbalimbali

Methali hii ina maana kuwa jambo moja linaweza kufanywa kwa namna mbalimbali.

 • Mchelea bahari si msafiri

Methali hii ina maana kuwa anayeiogopa bahari, hawezi kusafiri majini.

 • Mcheza hawi kiwete ngoma yataka matao

Methali hii ina maana kuwa kila shughuli anayoifanya binadamu inapaswa kufanywa kwa bidii na kujituma kwingi.

 • Mfa maji haishi kutapatapa

Methali hii ina maana kuwa mtu akipatwa na shida hutumia njia yoyote ili kujinusuru.

 • Mgaagaa na upwa, hali wali mkavu

Methali hii ina maana kuwa anayepita mahali penye riziki mara kwa mara aweza kubahatika.

 • Mkono mtupu haulambwi

Methali hii inamaanisha kuwa kama hauna kitu hutasaidika, lazima toa kitu ili upate kitu.

 • Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni

Hii methali ni kama mnyonge hana haki mpaka mwenye nguvu apende.

 • Mstahimilivu hula mbivu

Methali hii ina maana kuwa uvumilivu hadi mwisho unahitajika katika kufikia mema.

 • Mtaka cha mvunguni sharti ainame

Methali hii ina maana kuwa ili kupata mafanikio lazima kupitia misukosuko.

 • Mvumilivu hula mbivu

Methali hii ina maana kuwa mtu anayevumilia taabu na shida nyingi hupata mafaniko maishani.

 • Mwenda pole hajikwai

Methali hii ina maana kuwa ukifanya jambo kwa utaratibu utafanikiwa.

 • Mwenye nguvu mpishe

Methali hii ina maana kuwa si busara kupambana na mtu anayekuzidi uwezo.

 • Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu

Methali hii ina maana kuwa ni vizuri kushirikiana na binadamu wenzio.

 • Kula ni vyepesi lakini kulima ng’o

Methali ina maana kuwa kupata chakula ni rahisi kuliko kufanya kazi ili kupata chakula hicho.

Comments are closed.