Mifano 100 ya tashbihi

Posted by:

|

On:

|

Tashbihi ni lugha inayotumika kulinganisha vitu viwili vinavyofanana au kushabihiana. Inatumia viunganishi mithili ya, kama, mfano wa nk. Hii hap ani mifano ya tashbihi:

Mifano ya tashbihi

  1. Lala kama mfu
  2. Ng’ara sawa kama mwezi
  3. Mwoga mfano wa kunguru
  4. Simama wima mithili ya dandalo
  5. Ringa kama tausi
  6. Lazima kama ibada
  7. Mweusi mithili ya mkaa
  8. Mrembo mithili ya Malaika
  9. Cheka kama radi
  10. Maridadi kama kipepeo
  11. Nyeupe Kama theluji
  12. Mfupi Kama nyundo
  13. Mfupi kama mbilikimo
  14. Mrefu Kama mlingoti
  15. Mrefu kama ngamia
  16. Mrefu kama twiga
  17. Mweusi Kama makaa
  18. Bahati kama mtende
  19. Nukia kama ruhani
  20. Nuka kama beberu
  21. Tamu kama halua
  22. Nzito kama nanga
  23. Nyepesi kama unyoya
  24. Majuto kama ya firauni
  25. Kuiga kama kasuku.
  26. Tumainia kama tai
  27. Baridi kama barafu
  28. Kigeugeu kama kinyonga
  29. Mjanja Kama sungura
  30. Pendana Kama chanda na pete
  31. Tamu kama asali
  32. Kali kama Shubiri
  33. Tengana kama ardhi Na mbingu
  34. Mnene kama nguruwe
  35. Pendana kama ulimi na mate
  36. Polepole kama kobe
  37. Mweusi kama kizimwili
  38. Fuata mtu mfano wa kondoo
  39. Garagara kama mgonjwa
  40. Kuwa na hakika kama mauti
  41. Nata kama gundi
  42. Kuwa imara kama mwamba
  43. Mlafi kama fisi
  44. Mwaminifu kama njiwa
  45. Mjinga kama kondoo
  46. Mwenye bidii kama mchwa
  47. Mzima kama kigongo
  48. Tumbo kama kuruba
  49. Mkaidi kama punda
  50. Mkaidi kama kirongwe
  51. Laini kama hariri
  52. Laini kama pamba
  53. Mvumilivu kama mtumwa
  54. Ganda kama kigaga
  55. Msiri kama kaburi
  56. Msiri kama kobe
  57. Msiri kama usiku
  58. Msiri kama mvaa buibui
  59. Nata kama gundi
  60. Mwembamba kama ufito
  61. Mwembamba kama Uzi
  62. Mropokaji kama mlevi
  63. Baidika kama mbingu na ardhi
  64. Shabihiana kama kurwa na Doro
  65. Kigeugeu kama lumbwi
  66. Mnafiki kama panya
  67. Kung’aa kama dhahabu
  68. Angaza kama jua
  69. Laini kama hariri
  70. Tamu kama asali
  71. Nyeusi kama usiku wa manane
  72. Mrembo kama Malaika
  73. Jasiri kama simba
  74. Akili kama mchwa
  75. Chafu kama fugo
  76. Cheka kama malaika
  77. Chanua kama ua la asubuhi
  78. Chungwa kama mfungwa
  79. Dahadari kama anayekata roho
  80. Mwenye bashasha kama mapambazuko
  81. Mwenye bidii kama mchwa, nyuki
  82. Mwenye nguvu kama tembo
  83. Nyingi kama mchanga ufuoni
  84. Mkali kama simbabuka
  85. Mwenye maneno mengi kama chiriku
  86. Tulia kama maji mtungini
  87. Hasira kama za mkizi
  88. Fuatana kama kumbikumbi
  89. Sauti nzuri kama kinanda
  90. Kuzurura kama mbwakoko
  91. Kutapatapa kama samaki atolewapo majini
  92. Mpofu kama jongoo
  93. Tumbo kubwa kama kiriba.
  94. Paa kama moshi
  95. Maneno mengi kama chiriku
  96. Imara kama chuma cha pua
  97. Msahaulifu kama Nyati
  98. Kupenda kama moyo
  99. Wivu kama joka la mdimu
  100. Mpole kama kondoo

Comments are closed.