Mifano 25 ya vitanza ndimi

Vitanza ndimi ni  maneno yanayokaribiana na kuitanaitana kimatamshi na kumkanganya msomaji hasa anapoyatamka kwa haraka.

Mifano ya vitanza ndimi

  1. Kanga wa mahanga mwenye matanga anatangatanga tanga.
  2. Mchuuzi wa mchuzi wa juzi hajui mjusi wa jana.
  3. Katika kata ya mitakataka mkuu wa kata alikataa katakata takataka zisitupwe pahali tambarare tena.
  4. Shirika la reli la Seychelles lilishirikiana na shirika la reli la Senegal.
  5. Wape wale wanawali wale wali wao.
  6. Pema ni pema hujapopema ukipema si pema tena.
  7. Ni Nini kikusikitishacho?
  8. Kisikitiko kikusikitikisacho kisikitie.
  9. Msasa wa sasa wa Sasha una mkasa wa kasa si kasha.
  10. Susumila Shushushu mwenye sunzu si zuzu ila ana susu yenye shushu na ni chuchu.
  11. Ukivumbua alichovumbua Wambua akila kitumbua bila kukichambua sitakusumbua tena.
  12. Katibu Kata wa kata ya mkata alikataa katakata kukatakata takataka zilizokuwemo katika kata ya mkata.
  13. Mpambe mpeleke pembeni apambike ajue pembea ni mbeya.
  14. Bw Karama amaeandaa karamu iliomgarimu gharama kubwa.
  15. Baba alivua papa mkubwa baharini baada ya mvua kubwa kunyesha.
  16. Biketi aliketia kiketi alipofika kwa Keti wa Bi. Keti.
  17. Wali wa Liwali umeliwa na wana wa Liwali.
  18. Wale watu wa Liwali wala wali wa Liwali.
  19. Wanawali wa awali hawali wali wa awali ila wali wao.
  20. Nyanya Tanya alimkanya Tanya kutotawanya nyaya za nyanya ndani ya kaya.
  21. Shangaa kama shangazi aliyeshangaa baada ya kupoteza shanga kule tanga.
  22. Usishangae kama shangazi aliye nunua shanga kwa bei ya kushangaza.
  23. Wataita wa Taita wataita Wataita wa Taita.
  24. Sitasita kusisitisa kuwa sita na sita si tisa.
  25. Paliondokea mamba aliejibamba na kujigamba katika magamba ya wakamba huko ukambani.
Related Posts