Tanakali za sauti ni tamathali ya usemi ambayo hutumika kuigiza sauti au mlio wa kitu katika mazungumzo au maandishi na hivyo kufanya simulizi liwe hai zaidi.
Mifano ya tanakali za sauti
- Lia kwi! kwi! Kwi!
- Anguka pu!
- Tulia tulii!
- Cheka kwa! Kwa! Kwa!
- Tembea aste aste!
- Anguka kwa maji chubwi!
- Giza totoro!
- Kulewa chakari!
- Lala fofofo!
- Mweusi tititi!
- Funika gubigubi!
- Rarua raruraru!
- Kuanguka mchangani tifu!
- Nyeupe pe! pe!pe!
- Nyamaza jii!
- Bingirika bingiri bingiri!
- Tulia tuli!
- Mwaga mwaa!
- Kodoa kodokodo!
- Tembea aste aste!
- Tega sikio ndi!
- Pigwa kitutu!
- Anguka (mchangani) tifu!
- Tumbukia (majini) chubwi!
- Anguka (matopeni) tumbwi!
- Beba hobela hobela!
- Choka tiki!
- Kataa kata kata!
- Maliza fyuu!
- Zaba kofi pa!
- Nuka fe!
- Vunjika kacha!
- Zimia zi!
- Kuloa chepechepe!
- Teleza Parrr!
- Nyoka twaa!
- Mulika mwa!
- Tiririka tiriri!
- Ponea chupu chupu!
- Ng’ang’ana kukurukakara!
- Bebwa kindakindaki!
- Jikwatua kwatu kwatu!
- Jipodoa podo podo!