Mtaka cha mvunguni sharti ainame

Methali ya mtaka cha mvunguni sharti ainame ina maana kuwa ukitaka kitu fulani lazima uwe tayari kukisumbukia.

Maana zingine za mtaka cha mvunguni sharti ainame ni:

  • Ukitaka kufanikiwa maishani lazima utie bidii kwa lolote ulifanyalo.
  • Ukitaka kufaulu katika Jambo lolote lazima utie bidi.
  • Lazima ujifunge masombo ili ufaulu kukipata chenye unataka.
  • Tia bidii kwa kila jambo ambalo unalifanya ili uweze kufaulu.
  • Ukitaka kuwa na maisha bora, tumia nguvu zako ili upate mahitaji yako, uvivu huna nafasi.
  • Ili mtu afaulu katika kile anachofanya inabidi ajikakamue.

Methali sawa na mtaka cha mvunguni sharti ainame ni:

  • Mchumia juani hulia kivulini.
  • Mtegemea cha nduguye hufa masikini.
  • Atangaye sana na jua mwisho hujua.
  • Bidii hulipa.
  • Atangaye kizimani hunywa maji maenge.
  • Mgaagaa na upwa hali wali mkavu.
  • Achanikaye kwenye mpini hafi njaa.

Mfano kwa sentensi

Mtaka cha mvunguni sharti ainame. Mvulana huyo alijitolea kufanya kazi kwa bidii ili kupata elimu bora, na hatimaye alifanikiwa.

Related Posts