Hii ni ngeli ya majina ya viumbe wenye uhai kama vile watu, wanyama, ndege, wadudu, miungu, malaika n.k. Majina mengi katika ngeli ya A-WA huanza kwasauti M- kwa umoja na sauti WA- kwa wingi. Hatahivyo baadhi ya majina huchukua miundo tofauti.
Mifano ya nomino katika ngeli ya A – WA:
Wanadamu: mtoto, ndugu, msamaria, daktari, kiongozi
Wanyama: ng’ombe, mbuzi, swara, nyati, nguchiro
Ndege: bata, kuku, njiwa, mwewe, kipanga
Viumbe wa majini: samaki, papa, pweza, nyangumi na mamba
Wadudu: mende, mbu, kipepeo, nondo na nzi
Matakatifu wa kiimani: Mungu, Yesu, Mtume Mohammed na Malaika Israfili
Viumbe wasababishao zahama: jinni, pepo, na shatani
Mifano ya miundo ya ngeli ya A-WA;
KI-VI: Kiwete—Viwete, Kipofu – Vipofu, Kijana – Vijana, Kifarau – Vifaru, Kipepeo – Vipepeo, Kibogoyo – Vibogoyo
M-MI: Mtume—Mitume, Mkunga – Mikunga, Mkizi – Mikizi
CH-VY: Chura—Vyura
MU-WA: Muungwana – Waangwana, Muuguzi – Wauguzi
MW-WA: Mwalimu-Walimu, Mwizi – Wezi
M-WA: Mtoto – Watoto, Mtu- Watu, Mkunga – Wakunga, Mwanamke – Wanawake, Mwanamume, Wanaume, Mgonjwa – Wangonjwa, Mchungaji – Wachungaji
Ꝋ-MA: Nabii – Manabii, Waziri-Mawaziri, Daktari – Madaktari
Ꝋ- Ꝋ: kuku-kuku, papa-papa, mbuzi-mbuzi, popo-popo, chui-chui
Mifano katika sentensi
Umoja: Mwalimu ndiye amemkataza kuingia.
Wingi: Walimu ndio wamemkataza kuingia.
Umoja: Kibogoyo amefika.
Wingi: Vibogoyo wamefika.
Umoja: Malaika alimtembelea nabii wa kale.
Wingi: Malaika walitembelea manabii wa kale.
Umoja: Ngombe anakula.
Wingi: Ngombe wanakula.
Umoja: Mbuzi alikimbia.
Wingi: Mbuzi walikimbia.
Umoja: Daktari alimtibu.
Wingi: Madaktari walimtibu.
Umoja: Mtoto alilia.
Wingi: Watoto walilia.
Umoja: Chura aliruka.
Wingi: Chura waliruka.
2 responses to “Ngeli ya A-WA na mifano”