Silabi ni nini?
Silabi ni fungu la sauti linalotamkwa kwa pamoja kama fungu moja la sauti. Silabi inaweza kuwa na irabu moja au zaidi, au konsonanti moja au zaidi.
Silabi inaweza kuundwa na:
1. Irabu peke yake
Mifano:
Ua: U – a
Oa: O – a
2. konsonanti peke yake.
Mifano:
Mke: M – ke
Nje: N- je
3. konsonanti+irabu
Mifano:
Baba: Ba – ba
Peleka: Pe – le – ka
4. konsonanti+ konsonanti/ kiyeyusho+irabu
Mifano:
Mbali: Mba – li
Fyata: Fya – ta
Lizwa: Li -zwa
5. konsonanti + konsonanti + kiyeyusho na irabu
Mifano:
Jengwa: Je – ngwa
Mbweha: Mbwe – ha
6. Kiyeyusho + irabu
Mifano:
Waya: Wa – ya
Yale: Ya – le
7. silabi funge
Mifano:
Labda: Lab – da
Daftari: Daf – tari
Aina za silabi
Katika lugha ya kiswahili zipo aina kuu mbili za silabi.
Nazo ni:
Silabi wazi na silabi funge.
Silabi wazi
Silabi wazi ni ile yenye vokali na inayoishia kwa irabu. Na matamshi yake aghalabu hua ni ya kibantu.
Silabi wazi pia iko na aina zake:
1. Silabi Sahili
Hizi ni silabi ambazo huwa na irabu na konsonanti zikifuatana mtawalia.
Mfano:
baba, mama, kalamu, kula, lala n.k
2. Silabi mwambatano
Huwa na konsonanti mbili zinazotangulia irabu.
Mfano:
mwalimu, mtoto, mfawidhi, mwezi, mvua, mkate, ndoo nk.
3. Silabi changamano
Huwa na konsonanti tatu zinazotangulia irabu.
Mfano:
mpwa, mbwa, mbweha.
Silabi funge au mkopo
Hupatikana kwa maneno yasiyo na asili ya kibantu (kigeni).
Mfano:
Mufti, Sadakta, Daftari