Mtoto ni:
- Kiumbe mchanga anayezaliwa na mnyama au kiumbe yeyote mwenye uhai.
- Mtu ambaye hajatimiza umri wa utu uzima.
Ukubwa wa mtoto.
Kupata ukubwa wa mtoto tunazingatia sheria hizi za ukubwa wa nomino:
Nomino zenye kiambishi {m} mwanzoni na zenye silabi moja katika mzizi, kiambishi hicho hudondoshwa na kupachikwa kiambishi {ji}. Neno mtoto hufuata sheria hii ingawa neno ‘mtoto’ lina angalau silabi mbili.
Nomino zilizo na kiambishi {m} mwanzoni na silabi mbili au zaidi katika mzizi, kiambishi hicho hudondoshwa. Neno mtoto linaaza na kiambishi {m}, na lina angalau silabi mbili.
Kufuata sheria hizi za ukubwa wa nomino, ukubwa wa mtoto ni: toto au jitoto.
Mfano
Mtoto analia. Ukubwa wake ni; Toto linalia au jitoto linalia.
Ukubwa wa mtoto, toto au jitoto, haya maneno yanachukua ngeli ya {li -ya}, katika sentensi. Kumaanisha {li} katika umoja na {ya} katika wingi. Na pia unapachika kiambishi {ma} kupata wingi wa toto.
Kwa mfano
Toto/jitoto linalia. Matoto/majitoto yanalia.
Mifano katika sentensi:
- Toto hili linasumbua.
- Jitoto hili linapenda kukula.
- Alizaliwa akiwa jitoto kubwa sana.
Udogo wa mtoto.
Udogo wa mtoto ni kitoto ama kijitoto.
Mifano katika sentensi.
- Kijitoto hiki ni kidogo sana.
- Kitoto kinalia kwa sababu ya njaa.
- Kitoto changu kina njaa.