Maana ya visawe
Visawe ni maneno yaliyo na maana sawa.
Mifano ya visawe
- Adui – Visawe vya neno “adui” ni “hasimu” na “hasidi”.
- Msichana – Visawe vya msichana ni: Binti, Kidosho, Banati, Kipusa, Gashi
- Mvulana – Visawe vya mvulana ni: Mtanashati, Ghulamu, Janadume, Mvuli, Barobaro, Shababi
- Mama – Visawe vya mama ni: Nina, Nyoko
- Barabara – Kisawe cha barabara ya njia ni baraste au tariki, Kisawe cha barabara ya bila kasoro ni sawasawa.
- Kinyonga – Kisawe cha Kinyonga ni Lumbwi.
- Daktari – Visawe vya Daktari ni: Muuguzi, Mganga, Tabibu
- Heshima – Kisawe cha heshima ni staha
- Pesa – Visawe vya pesa ni: peni, darahima, fulusi, fedha, hela
- Mnyama – Kisawe cha mnyama ni hayawani
- Maskini – Kisawe cha maskini ni fukara
- Mwizi – Visawe vya mwizi ni: Luja, Mwivi, n.k
- Binadamu – Visawe vya binadamu ni: Insi, Mja, Mtu, Mahuluki
- Kipindupindu – Kisawe cha kipindupindu ni waba
- Mwanafunzi – Kisawe cha mwanafunzi ni: Mwanagenzi, Mwanafuu
- Dalili – Kisawe cha dalili ni ishara
- Msitu – Kisawe cha msitu ni pori
- Lebasi – Kisawe cha lebasi ni vazi, nguo
- Zaraa – Kisawe cha zaraa ni kilimo
- Mwalimu – Visawe vya mwalimu ni: Mkufunzi, Mdarisi
Mifano mingine ya visawe ni:
- Ardhi=Dunia
- Ari=Nia
- Aibu=Soni
- Azma=Makusudio
- Binti=Msichana
- Chakula=Mlo
- Chanzo=Sababu
- Cheti=Hati
- Chuana=Shindana
- Chubua=Chuna
- Chubuko=Jeraha
- Chumvi=Munyu
- Duara=Mviringo
- Dunia=Ulimwengu
- Familia=Kaya
- Fedha=Hela/Pesa
- Fukara=Maskini
- Gari Moshi=Treni
- Ghasia=Fujo
- Ghiliba=Hila
- Godoro=Tandiko
- Hitimaye=Mwishowe
- Herufi=Hati
- Hesabu=Hisabati
- Hodari=Bingwa
- Idhini=Ruhusa
- Jogoo=Jimbi
- Jokofu=Friji
- Kandanda=Soka
- Kenda=Tisa
- Kichaa=Mwendawazimu
- Kileo=Pombe
- Kimada=Hawara
- Kiranja=Kiongozi
- Kivumbi=Fujo
- Kopoa=Zaa
- Kongoro=Gema
- Labda=Huenda
- Labeka!=Abee!/Naam!
- Laghai=Danganya
- Lisanj=Ulimi
- Majira=Wakati
- Manii=Shahawa
- Masalia=Mabaki
- Mashaka=Tabu
- Mbio=Kasi
- Mchoyo=Bahili
- Mdomo=Kinywa
- Mlolongo=Foleni
- Motokaa=Gari
- Msimu=Majira
- Mtima=Moyo
- Mtindi=Maziwa Mgando
- Mtindo=Staili
- Mtu=Binadamu
- Muda=Wakati
- Mvuli=Mvulana
- Nahodha=Kapteni
- Nakshi=Urembo
- Ndoa=Chuo
- Ndondi=Masumbwi
- Ndovu=Tembo
- Nguo=Mavazi
- Nguzo=Kanuni
- Nia=Lengo
- Nuru=Mng’ao
- Nyanya=Bibi
- Nyati=Mbogo
- Ongea=Sema/Zungumza
- Pombe=Mtindi
- Raba=Kifutio
- Rabana=Mola
- Rafiki=Sahibu/Swahibu
- Rehani=Poni
- Rubani=Kapteni
- Rundika=Tufika
- Rushwa=Hongo
- Saka=Winda
- Sala=Dua
- Samani=Fanicha
- Shika=Kamata
- Shujaa=Jasiri
- Spika=Kipaza sauti
- Starehe=Tamasha
- Sura=Uso
- Tafrija=Sherehe
- Terevisheni=Runinga
- Thenashara=Kumi na mbili
- Tumbiri=Ngedere
- Ugonjwa=Maradhi
- Uja=Ubinadamu
- Ukaidi=Ujeuri
- Ukumbi=Surua
- Ukuta=Kiambaza
- Ukwasi=Utajiri
- Upara=Kidazi
- Urembo=Umaridadi
- Vamio=Shambulio
- Vifijo=Vigelegele
- Vunja=Pasua
- Vurugu=Fujo
- Vuu=Ghafla
- Nyema=Vizuri
- Wajihi=Uso
- Wakala=Ajenti
- Waraka=Barua
- Waza=Fikiri
- Weupe=Mwangaza
- Weusi=Giza
- Wiki=Juma
- Winda=Nepi
- Wivu=Husuda
- Chupi=Kocho
- Karai=Beseni/Dishi
- Mamba=Kenge
Visawe pdf
Hii hapa ni pdf ya mifano ya visawe unaenza download: