Visawe na mifano

Posted by:

|

On:

|

Maana ya visawe

Visawe ni maneno yaliyo na maana sawa.

Mifano ya visawe

 • Adui – Visawe vya neno “adui” ni “hasimu” na “hasidi”.
 • Msichana – Visawe vya msichana ni: Binti, Kidosho, Banati, Kipusa, Gashi
 • Mvulana – Visawe vya mvulana ni: Mtanashati, Ghulamu, Janadume, Mvuli, Barobaro, Shababi
 • Mama – Visawe vya mama ni: Nina, Nyoko
 • Barabara – Kisawe cha barabara ya njia ni baraste au tariki, Kisawe cha barabara ya bila kasoro ni sawasawa.
 • Kinyonga – Kisawe cha Kinyonga ni Lumbwi.
 • Daktari – Visawe vya Daktari ni: Muuguzi, Mganga, Tabibu
 • Heshima – Kisawe cha heshima ni staha
 • Pesa – Visawe vya pesa ni: peni, darahima, fulusi, fedha, hela
 • Mnyama – Kisawe cha mnyama ni hayawani
 • Maskini – Kisawe cha maskini ni fukara
 • Mwizi – Visawe vya mwizi ni: Luja, Mwivi, n.k
 • Binadamu – Visawe vya binadamu ni: Insi, Mja, Mtu, Mahuluki
 • Kipindupindu – Kisawe cha kipindupindu ni waba
 • Mwanafunzi – Kisawe cha mwanafunzi ni: Mwanagenzi, Mwanafuu
 • Dalili – Kisawe cha dalili ni ishara
 • Msitu – Kisawe cha msitu ni pori
 • Lebasi – Kisawe cha lebasi ni vazi, nguo
 • Zaraa – Kisawe cha zaraa ni kilimo
 • Mwalimu – Visawe vya mwalimu ni: Mkufunzi, Mdarisi

Mifano mingine ya visawe ni:

 • Ardhi=Dunia
 • Ari=Nia
 • Aibu=Soni
 • Azma=Makusudio
 • Binti=Msichana
 • Chakula=Mlo
 • Chanzo=Sababu
 • Cheti=Hati
 • Chuana=Shindana
 • Chubua=Chuna
 • Chubuko=Jeraha
 • Chumvi=Munyu
 • Duara=Mviringo
 • Dunia=Ulimwengu
 • Familia=Kaya
 • Fedha=Hela/Pesa
 • Fukara=Maskini
 • Gari Moshi=Treni
 • Ghasia=Fujo
 • Ghiliba=Hila
 • Godoro=Tandiko
 • Hitimaye=Mwishowe
 • Herufi=Hati
 • Hesabu=Hisabati
 • Hodari=Bingwa
 • Idhini=Ruhusa
 • Jogoo=Jimbi
 • Jokofu=Friji
 • Kandanda=Soka
 • Kenda=Tisa
 • Kichaa=Mwendawazimu
 • Kileo=Pombe
 • Kimada=Hawara
 • Kiranja=Kiongozi
 • Kivumbi=Fujo
 • Kopoa=Zaa
 • Kongoro=Gema
 • Labda=Huenda
 • Labeka!=Abee!/Naam!
 • Laghai=Danganya
 • Lisanj=Ulimi
 • Majira=Wakati
 • Manii=Shahawa
 • Masalia=Mabaki
 • Mashaka=Tabu
 • Mbio=Kasi
 • Mchoyo=Bahili
 • Mdomo=Kinywa
 • Mlolongo=Foleni
 • Motokaa=Gari
 • Msimu=Majira
 • Mtima=Moyo
 • Mtindi=Maziwa Mgando
 • Mtindo=Staili
 • Mtu=Binadamu
 • Muda=Wakati
 • Mvuli=Mvulana
 • Nahodha=Kapteni
 • Nakshi=Urembo
 • Ndoa=Chuo
 • Ndondi=Masumbwi
 • Ndovu=Tembo
 • Nguo=Mavazi
 • Nguzo=Kanuni
 • Nia=Lengo
 • Nuru=Mng’ao
 • Nyanya=Bibi
 • Nyati=Mbogo
 • Ongea=Sema/Zungumza
 • Pombe=Mtindi
 • Raba=Kifutio
 • Rabana=Mola
 • Rafiki=Sahibu/Swahibu
 • Rehani=Poni
 • Rubani=Kapteni
 • Rundika=Tufika
 • Rushwa=Hongo
 • Saka=Winda
 • Sala=Dua
 • Samani=Fanicha
 • Shika=Kamata
 • Shujaa=Jasiri
 • Spika=Kipaza sauti
 • Starehe=Tamasha
 • Sura=Uso
 • Tafrija=Sherehe
 • Terevisheni=Runinga
 • Thenashara=Kumi na mbili
 • Tumbiri=Ngedere
 • Ugonjwa=Maradhi
 • Uja=Ubinadamu
 • Ukaidi=Ujeuri
 • Ukumbi=Surua
 • Ukuta=Kiambaza
 • Ukwasi=Utajiri
 • Upara=Kidazi
 • Urembo=Umaridadi
 • Vamio=Shambulio
 • Vifijo=Vigelegele
 • Vunja=Pasua
 • Vurugu=Fujo
 • Vuu=Ghafla
 • Nyema=Vizuri
 • Wajihi=Uso
 • Wakala=Ajenti
 • Waraka=Barua
 • Waza=Fikiri
 • Weupe=Mwangaza
 • Weusi=Giza
 • Wiki=Juma
 • Winda=Nepi
 • Wivu=Husuda
 • Chupi=Kocho
 • Karai=Beseni/Dishi
 • Mamba=Kenge

Visawe pdf

Hii hapa ni pdf ya mifano ya visawe unaenza download: