Mistari ya biblia kuhusu msiba na za kutia moyo.

Posted by:

|

On:

|

Maisha ni milima na mabonde, huzuni na furaha. Ndio maana katika kitabu cha Mhubiri 3:1-8, imeandikwa kuwa:

Kila kitu kina majira yake, kila jambo duniani lina wakati wake: Wakati wa kuzaliwa na wakati wa kufa; wakati wa kupanda na wakati wa kuvuna kilichopandwa; wakati wa kuua na wakati wa kuponya; wakati wa kubomoa na wakati wa kujenga; wakati wa kulia na wakati wa kucheka; wakati wa kuomboleza na wakati wa kucheza; wakati wa kutupa mawe na wakati wa kuyakusanya mawe pamoja; wakati wa kukumbatia na wakati wa kuacha kukumbatia; wakati wa kutafuta na wakati wa kupoteza; wakati wa kuhifadhi na wakati wa kutupa; wakati wa kurarua na wakati wa kushona; wakati wa kukaa kimya na wakati wa kuongea; wakati wa kupenda na wakati wa kuchukia; wakati wa vita na wakati wa amani.

Ikiwa sahii uko na msiba k.v majonzi, kufiwa, shida n.k, hizi ni mistari ya biblia kuhusu msiba za kukutia moyo.

Mistari ya biblia kuhusu msiba za kukutia moyo.

Zaburi 34:18 BHN

Mwenyezi-Mungu yu karibu na waliokufa moyo; huwaokoa wote waliokata tamaa kabisa.

Mathayo 5:4 BHN

Heri walio na huzuni, maana watafarijiwa.

Ufunuo 21:4 BHN

Yeye atayafuta machozi yao yote; maana kifo hakitakuwako tena, wala uchungu, wala kilio, wala maumivu; maana ile hali ya kale imepita!”

Zaburi 23:4 BHN

Nijapopita katika bonde la giza kuu la kifo, sitaogopa hatari yoyote, maana wewe ee Mwenyezi-Mungu u pamoja nami; gongo lako na fimbo yako vyanilinda.

Warumi 8:38-39 SRUV

Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.

Zaburi 18:2 BHN

Mwenyezi-Mungu ni mwamba wangu, ngome yangu na mkombozi wangu; Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia usalama; ngao yangu, nguvu za wokovu wangu na ngome yangu.

Yohana 14:27 SRUV

Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga.

1 Petro 5:7 SRUV

Huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.

Zaburi 34:17 BHN

Waadilifu wakimlilia Mwenyezi-Mungu yeye huwasikia, na kuwaokoa katika taabu zao zote.

Mhubiri 3:1-8 BHN

Kila kitu kina majira yake, kila jambo duniani lina wakati wake.

Yohana 16:33 NEN

Nimewaambia mambo haya, ili mpate kuwa na amani mkiwa ndani yangu. Ulimwenguni mtapata dhiki. Lakini jipeni moyo, kwa maana mimi nimeushinda ulimwengu.”

Zaburi 29:11 BHN

Mwenyezi-Mungu na awape watu wake nguvu! Mwenyezi-Mungu na awabariki watu wake kwa amani!

Warumi 8:28 SRUV

Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.

Isaya 41:13 SRUV

Kwa maana mimi, BWANA, Mungu wako, nitakushika mkono wako wa kulia, nikikuambia, Usiogope; mimi nitakusaidia.

Yohana 11:25-26 SRUV

Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, hata akifa, atakuwa anaishi; naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je! Unayasadiki hayo?

Zaburi 9:9 BHN

Mwenyezi-Mungu ni ngome ya watu wanaoonewa; yeye ni ngome nyakati za taabu.

Zaburi 73:26 BHN

Hata nikikosa nguvu mwilini na rohoni, wewe, ee Mungu, u mwamba wangu; riziki yangu kuu ni wewe milele.

Isaya 43:2 BHN

Mkipita katika mafuriko, mimi nitakuwa pamoja nanyi; mkipita katika mito, haitawashinda nguvu. Mkitembea katika moto, hamtaunguzwa; mwali wa moto hautawaunguza.

Zaburi 23:1-3 BHN

Mwenyezi-Mungu ni mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu. Hunipumzisha kwenye malisho mabichi; huniongoza kando ya maji matulivu, na kuirudishia nafsi yangu nguvu mpya. Huniongoza katika njia sawa kwa hisani yake.

Isaya 40:31 BHN

Lakini wote wanaomtumainia Mwenyezi-Mungu, watapata nguvu mpya. Watapanda juu kwa mabawa kama tai; watakimbia bila kuchoka; watatembea bila kulegea.

Yohana 14:1 SRUV

Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi.

2 Wakorintho 4:16-17 SRUV

Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku. Maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda mfupi tu, yatuandalia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana.

Methali 3:5-6 BHN

Mtumaini Mwenyezi-Mungu kwa moyo wako wote, wala usitegemee akili zako mwenyewe. Umtambue Mungu katika kila ufanyalo, naye atazinyosha njia zako.

Zaburi 86:15 BHN

Lakini wewe Bwana, ni Mungu wa rehema na huruma; wewe ni mvumilivu, mwingi wa fadhili na uaminifu.

Nahumu 1:7 BHN

Mwenyezi-Mungu ni mwema, yeye ni ngome ya usalama wakati wa taabu. Yeye huwalinda wote wanaokimbilia usalama kwake.

2 Timotheo 4:7 SRUVDC

Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda.

Zaburi 23:6 SRUV

Hakika wema na fadhili zitanifuata Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa BWANA milele.

Warumi 8:28 SRUV

Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.

Zaburi 116:5 BHN

Mwenyezi-Mungu amejaa wema na uaminifu; Mungu wetu ni mwenye huruma.

Warumi 15:13 SRUV

Basi Mungu wa tumaini na awajaze ninyi furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mtakatifu.