Mistari ya shukrani katika biblia

Posted by:

|

On:

|

Ikiwa unatafuta vifungu vya biblia vya shukrani, umefika ndipo. Katika Makala haya tumekupa mistari kutoka kwa biblia ya kupiga shukrani kwa Mungu kwa mengi ambayo amekutendea.

Mistari ya shukrani katika biblia

1 Wathesalonike 5:18 NEN

Shukuruni kwa kila jambo, kwa maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu kwa ajili yenu katika Kristo Yesu.

Zaburi 100:4 BHN

Pitieni milango ya hekalu lake kwa shukrani, ingieni katika nyua zake kwa sifa. Mshukuruni na kulisifu jina lake.

Wakolosai 3:17 SRUV

Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kupitia kwake.

Wafilipi 4:6 SRUV

Msijisumbue kwa neno lolote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.

Zaburi 107:1 BHN

Mshukuruni Mwenyezi-Mungu kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake zadumu milele!

Waefeso 5:20 BHN

Mshukuruni Mungu Baba daima kwa ajili ya yote, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo.

Zaburi 118:1 BHN

Mshukuruni Mwenyezi-Mungu, kwa kuwa ni mwema, kwa maana fadhili zake zadumu milele.

Yakobo 1:17 (NIV)

Kila kipawa chema na kila zawadi kamilifu hutoka mbinguni, ikishuka kutoka kwa Baba wa nuru za mbinguni ambaye habadiliki kama kivuli.

1 Mambo ya Nyakati 16:34 BHN

Mshukuruni Mwenyezi-Mungu kwa kuwa ni mwema, kwa maana fadhili zake zadumu milele!

Zaburi 136:1 SRUV

Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

Wakolosai 4:2 BHN

Dumuni katika sala, na mnaposali muwe waangalifu, mkimshukuru Mungu.

Mistari ya biblia ya kumshukuru mungu

Zaburi 30:12 BHN

Mimi nitakusifu wala sitakaa kimya. Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu nitakushukuru milele.

Zaburi 95:2-3

2 Tuje mbele zake kwa shukrani, Tumfanyie shangwe kwa zaburi. 3 Kwa kuwa BWANA ni Mungu mkuu,

Na Mfalme mkuu juu ya miungu yote.

2 Wakorintho 9:15 BHN

Tumshukuru Mungu kwa ajili ya zawadi yake isiyo na kifani!

Zaburi 107:8-9 Biblia Habari Njema (BHN)

Mshukuruni Mwenyezi-Mungu kwa fadhili zake; kwa sababu ya maajabu aliyowatendea binadamu. Yeye huwatosheleza walio na kiu; na wenye njaa huwashibisha mema.

Wakolosai 3:15 BHN

Nayo amani ya Kristo itawale mioyoni mwenu; maana kwa ajili hiyo nyinyi mmeitwa katika mwili huo mmoja. Tena muwe na shukrani!

Zaburi 28:7 BHN

Mwenyezi-Mungu ndiye nguvu yangu na ngao yangu; tegemeo la moyo wangu limo kwake. Amenisaidia nami nikashangilia kwa moyo; kwa wimbo wangu ninamshukuru.

Zaburi 69:30 BHN

Kwa wimbo nitalisifu jina la Mungu, nitamtukuza kwa shukrani.

1 Wathesalonike 5:16-18 BHN

Furahini daima, salini kila wakati na kuwa na shukrani katika kila hali. Hayo ndiyo anayotaka Mungu kwenu katika kuungana kwenu na Kristo Yesu.

Zaburi 147:7 BHN

Mwimbieni Mwenyezi-Mungu nyimbo za shukrani, mpigieni kinubi Mungu wetu!

Zaburi 95:2 SRUV

Tuje mbele zake kwa shukrani, Tumfanyie shangwe kwa zaburi.