Kumkatia na kumuingiza dem box si jambo rahisi. Kunaweza kukusisimua na kukushtua. Hata hivyo, usiogope, kwa maana kumtongoza dem mara nyingi ni kujiamini, kumpatia respect, na kuwa mwenyewe, usiwe fake. Hapa chini tutakueleza jinsi ya kutongonza na kumkatia dem na umuingize kwa box. Kwa kufuata hatua hizi, unaweza kuongeza nafasi zako za kushinda moyo wake na pia kujenga uhusiano wa maana na wa kudumu.
Jinsi ya kutongoza
Hizi ni tips za kukatia na kumtongoza dem yeyote.
Tips za kukatia
Kuwa msafi na uvae mavazi mazuri
Hii ni njia rahisi ya kumfanya msichana avutiwe na wewe zaidi. Oga na ujitie perfume kiasi ili mwili wako unukie safi, na uvae nguo ambazo ukivaa unafeel confident na kuvutia.
Kufanya mambo madogo kama vile kusugua meno yako na kuweka mavazi mazuri kunaongeza uwezekano mkubwa wa kuvutia umakini wa msichana.
Mtazame machoni ili kuvutia umakini wake.
Unapomshika msichana akikutazama, jaribu kudumisha mtazamo wa macho naye kwa sekunde kadhaa kabla ya kutabasamu na kutazama pembeni. Hilo litamdokezea kwamba unampenda kikweli na kumfanya apendezwe zaidi nawe. Unapozungumza naye, mtazame machoni, usiangalie kando ama chini. Jaribu kuzuia kumtazama machoni pake kwa zaidi ya sekunde 3, kwani hii kutamfanya akuwe na wasiwasi
Kujiamini
Kujiamini ni sumaku ya kumnasa dem. Kabla ya kumkaribia, jitahidi kujenga hali ya kujiamini. Amini katika thamani yako, tambua uwezo wako, na ufurahie jinsi ulivyo. Kujiamini itakufanya uvutie zaidi na dem atafeel comfortable karibu na wewe.
Tafuta ishara za kumkaribia
Kabla ya kuwa na wasiwasi juu ya kile utakachosema au kufanya ili kumkaribia msichana, kwanza unahitaji kuelewa ni wakati gani unapaswa kumkaribia. Mara nyingi, timing ya kumkaribia ni muhimu kwa sababu dem anaweza kukataa ama kukubali kulingana na mazingira.
Hapa kuna mifano ya wakati unapaswa na yenye hupaswi kumkaribia msichana:
- Mkaribie msichana ikiwa ameketi/amesimama na anaonekana ametulia. Wasichana ambao wako katika hali nzuri na wanaonyesha utulivu huwa tayari kuwa na mazungumzo.
- Mkaribie ikiwa umemwona akikutazama mara kadhaa au anatabasamu ukimwangalia. Hili likitokea, huenda anavutiwa nawe na anataka uanzishe mazungumzo.
- Usimkaribie msichana ikiwa anaonekana kukasirika. Uwezekano ni kwamba ikiwa ana siku mbaya, hatakujibu vyema.
- Usimkaribie msichana ikiwa anajishughulisha sana na jambo fulani. Kumkatiza hakutaleta mwonekano mzuri.
Mkaribie kutoka upande
Wanawake kwa kawaida huwa macho wanapozungukwa na watu wasiowajua. Kumkaribia mwanamke kutoka nyuma au mbele kunaweza kutisha kwa sababu anaogopa kushambuliwa. Badala yake, mwendee msichana polepole kutoka pembeni ili aweze kukuona ukija na kujiandaa kwa uwepo wako, badala ya kushtushwa na wewe.
Toa lugha chanya ya mwili kuonyesha kwamba ana umakini wako.
Unaweza kufanya hivyo kwa kusimama tu au kukaa karibu naye. Tabasamu sana unapokuwa karibu na yeye, na zingatia ishara zozote anazotoa ili kuona kama anakupenda pia.
Thibitisha unastahili kuzungumza naye.
Ukimkaribia msichana anakuwa na maswali kadhaa akilini mwake kama vile: huyu anataka nini kutoka kwangu? Lakini kadiri utakavyoweza kumsaidia kujibu maswali kama hayo kwa haraka, ndivyo atakavyofurahishwa nawe na kuwa tayari kushiriki katika mazungumzo. Hapa kuna mifano ya uaanzilishi wa mazungumzo na msichana:
Muombe ushauri kilingana na mzingira uliomkuta, kama ulimkuta akitembea unaenza muuliza “Ni wapi pazuri pa kula hapa?”ama umulize direction ya place fulani. Kama ni kwa shule unaenza muuliza “Unapenda unit gani?” ama “Mtihani ulikupelekaje?” Hii ni njia rahisi ya kuanzisha mazungumzo na msichana. Pia unaweza kumuliza akufanyie jambo, kama “Unaweza nisaidia na kalamu?” ama “Nishikia hii bag nifunge kiatu.”
Mwambie kwamba anavutia.
Mwambie kile unachopenda kumhusu, sio kuzingatia tu sura. Kwa mfano, unaweza kumwambia kwamba unapenda utu wake, kama vile ukimuuliza ushauri na akupatie, mshukuru na umwambie vile yeye ako na utu bora, au mwambie kwa nini unafikiri yeye ni bora katika kazi yake au shuleni.
Sema kitu kama, “Una tabasamu nzuri,” au “Asante kwa kunisadia, wewe ni msichana mwenye utu mzuri.” ama “Wewe ni mrembo sana.”
Ukitaka maneno matamu zaidi ya kumwambia soma hii misemo ya mapenzi.
Heshima ni muhimu
Mkaribie kwa heshima ya kweli. Heshimu nafasi yake binafsi, maoni na maamuzi. Msikiliza anapozungumza, na uonyeshe unapendezwa kikweli na yeye. Heshima huunda msingi wa uaminifu, ambao ni kipengele muhimu cha uhusiano wowote wenye mafanikio.
Uhalisi: Kuwa wewe
Kuwa wa kweli. Mwambie jina lako, unatoka wapi na unafanya nini kimaisha. Kujifanya mtu ambaye sio wewe haiwezi kuwa kwa muda mrefu, atagundua unamdanganya na akuache. Mwonyeshe ubinafsi wako wa kweli – mambo yanayokuvutia, na mambo unayopenda. Kuwa mkweli hukuza uhusiano wa kimaana, hata kama huyo dem hatakupenda baadaye kutakusaidia kumpata msichana anayekuthamini kwa jinsi ulivyo.
Mazungumzo ya Kuvutia na yeye
Anzisha mazungumzo yenye maana. Muulize jina lake, anatoka wapi na anafanya nini kujishughuliza kimaisha. Mulize maswali ya wazi ambayo yanamtia azungumze na wewe. Kwa mfano ukijua anapenda nini, muliza kwa nini ili akuelezee zaidi. Hii itakusaidia kuendeleza mazungumzo na yeye.
Muombe namba yake
Baada ya kujuana kiasi, muombe namba yake ya simu ndio muongee zaidi na ikuwe rahisi kukutana baadaye. Kwa mfano unaenza mwambia kuwa “Nisaidie na namba yako ya simu tuongee zaidi baadaye.”
Wasiliana naye mara kwa mara ili kujuana vizuri zaidi.
Ukishachukua namba yake, hakikisha unawasiliana naye mara kwa mara. Kwa kuzungumza naye, utajifunza zaidi kumhusu na utamwonyesha kwamba unamfikiria.
Mtumie SMS rahisi inayosema, “Natumai una siku njema,” au “Una mipango gani ya wikendi?”
Ukitaka SMS zaidi za kumtumia soma hizi SMS za mapenzi.
Muulize maswali kadhaa kumhusu ili kuonyesha kwamba unavutiwa naye.
Sio tu kwamba hii itakusaidia kumjua zaidi, lakini pia atathamini juhudi unazofanya kumjua. Muulize maswali kuhusu shule au kazi, familia yake, na mambo anayopenda.
Muulize kile anachopenda kufanya wikendi ama akiwa free, mahali anapopenda kwenda kutulia na vitu vinginevyo.
Ukianzisha mazungumzo ya aina hii, anaweza hata kukuuliza maswali kukuhusu pia, hivi ataonyesha kwamba angependa kukujua pia.
Unda uhusiano wa maana kwa kutafuta vitu mnazopenda wote.
Hii inaweza kuwa ninyi nyote mnapenda michezo au mnafanya unit moja shuleni au kuwatch movie. Kuzungumzia mambo mnayopenda wote kutaimarisha uhusiano wenu, na pia kutakupa mawazo ya mambo mnayoweza kufanya pamoja.
Ikiwa nyinyi wawili mnapenda michezo, mnaweza panga kwenda kuwatch mpira ama michezo yoyote inayochezwa karibu.
Labda yote mnapenda kusoma, kutazama sinema za kutisha, au kuhike. Panga mfanye hilo jambo mnaopenda.
Mwambie jinsi unavyohisi kumhusu.
Kumjulisha jinsi unavyojihisi kutafanya nia yako iwe wazi zaidi utakapo muuliza awe mpenzi wako. Mwambie jinsi unavyohisi kumhusu, mwulize jinsi anavyohisi kukuhusu pia.
Unaweza kumwambia, “Ninapenda sana vile unanifanya nihisi kuwa mtu wa maana.”
Jaribu kuzuia kufanya hivi kwa text ama SMS. Kumwambia msichana jinsi unavyohisi ana kwa ana kutafanya wakati huu kuwa maalum zaidi kwa nyinyi wawili.
Jinsi ya kumuuliza msichana awe mpenzi wako
Ikiwezekana muulize ana kwa ana. Ni vyema kuepuka kumuuliza msichana awe mpenzi wako kupitia SMS au mitandao ya kijamii—kwa sababu hutaweza kuona hisia zake za kweli. Mkikutana, pata mda bora wa kumuuliza awe mpenzi wako, muulize swali kama “Je, ungependa kuwa mpenzi wangu?”
Ongeza mguso zaidi ikiwa unamuuliza kwa SMS. Weka maandishi yako rahisi kwa kusema kitu kama, “Je, utakuwa mpenzi wangu?” na kisha kuongeza emoji nzuri, GIF au picha. Unaweza pia kupata ubunifu zaidi na SMS yako kwa kumwambia kile unachopenda kumhusu.
Unaweza kutuma ujumbe kama, “Nimependezwa nawe tangu tulipokutana—je utakuwa mpenzi wangu?”
Mwandikie barua ya kimahaba. Ikiwa una woga sana wa kumuuliza ana kwa ana au unataka kueleza hisia zako kwa undani zaidi, barua ni njia nzuri sana ya kumuuliza awe mpenzi wako. Andika kila kitu ambacho ungependa kumwambia, ukiongeza swali kama “Je, utakuwa mpenzi wangu?” karibu na mwisho.
Hizi hapa ni barua za mapenzi unaweza kumtumia.
Heshimu uamuzi wake ikiwa atakukataa.
Jaribu kutoichukulia kibinafsi ikiwa hataki kuwa mpenzi wako. Chukua muda wako kupoa kutoka kwa hisia hizo za kukataliwa, na ujue kwamba kuna msichana mwingine atakupenda vile uko.