Tips za mapenzi za kuongeza upendo kwa uhusiano

Posted by:

|

On:

|

Mara nyingi si kwa kukosa upendo ambapo mahusiano mengi huvunjika. Hapa kuna tips 7 za  mapenzi za kuongeza nguvu na upendo katika uhusiano.

Tips za kuongeza mapenzi

Tips za mapenzi

Weka mapenzi ya kimwili hai katika uhusiano

Ingawa ngono mara nyingi ni msingi wa uhusiano, haipaswi kuwa njia pekee ya mapenzi ya kimwili. Kumgusa mpenzi wako mara kwa mara kwa upendo, kumshika mikono, kumkumbatia, kumbusu—ni muhimu vile vile.

Msikilize mpenzi wako

Ikiwa unaweza kujifunza kusikiliza kwa njia ambayo inamfanya mtu mwingine ajisikie kuwa anathaminiwa na kueleweka, unaweza kujenga uhusiano wa kina na wenye nguvu.

Ukimsikiliza mpenzi wako haimaanishi kwamba unapaswa kukubaliana na kila anachosema au kubadilisha mawazo yako. Lakini itakusaidia kupata maoni yake ambayo yanaweza kukusaidia kutatua mzozo kati yenu.

Tatua changamoto pamoja

Mojawapo ya njia bora za kuimarisha upendo katika uhusiano ni kutatua changamoto pamoja. Ikiwa unapitia jambo gumu kwa ndoa-labda unajaribu kupata mtoto au unashughulikia deni, mwambie mpenzi wako na mlitatue kama timu. Ikiwa unatatizika kama mtu binafsi acha mwenzako akusaidie. Mkisaidiana kwa changamoto zozote zitakazojitokeza kwa uhusiano kunaweza kuongeza upendo wenu.

Mthamini mpenzi wako

Hata kama mmekuwa na mpenzi wako kwa muda mrefu, inaweza kuwa unamchukulia mwenzi wako kama mtu wa kawaida. Lakini kama unataka kuongenza upendo kwa uhusiano, mthamini huyo mpenzi. Mwambie asante akikufanyia jambo ambalo unataka, mwambie unampenda, wakati mwingine mtumie jumbe fupi za mapenzi. Mjulishe mpenzi wako ni kiasi gani anachomaanisha kwako ili asijisikie kuwa amechukuliwa kama mtu wa kawaida.

Jifunze kusamehe

Usiruhusu chuki ijenge kwa uhusiano wenu. Kuweka kinyongo kutakurudisha nyuma na kuumiza uhusiano wako kwa muda mrefu. Msamaha ni ufunguo wa uhusiano wowote wa kuwa na mapenzi ya nguvu. Hivyo ikiwa kuna kitu mpenzi wako alifanya na kikaleta mzozo kati yenu, msamehe na usahau. Watu hufanya makosa na hakuna mtu mkamilivu, hata wewe kwa njia moja ama nyingine hukosa.

Kuwa na  mwenye huruma.

Wakati mwingine unaweza kushawishika kumpiga mwenzi wako unapohisi kuudhika. Hata hivyo, unaweza kuwasilisha hisia zako bila kuwa mkorofi.

Upendo wenye huruma ni kinyume cha kukosa subira, kuwa mfidhuli, na mwenye hasira. Ukiwa na uhuruma kwa mwenzio utatambua kuwa mwenzako pia ana matamanio na mapambano yake binafsi.

Kila uhusiano ni kama mti mchanga ambao unahitaji kulindwa na kunyunyusiwa maji kila mara ndio ukuwe. Kwa hivyo ukiuchukulia uhusiano wako kuwa mti mchanga kunaweza kuongeza motisha yako ya kukua na uhuruma na subira katika uhusiano.

Jifunze kutoa na kupokea katika uhusiano wako

Ikiwa unatarajia kupata kile unachotaka kila wakati kwa uhusiano, unajiweka katika hali mbaya kwa uhusiano. Mahusiano mazuri ni yale ya kupeana pia wewe kwa mwenziwe, si kila wakati kupokea na haumpatii chochote mwenzi wako. Hata hivyo, inachukua kujituma pande zote kwa uhusiano ili kuhakikisha kwamba kuna ubadilishanaji unaofaa.

Tambua kile ambacho ni muhimu kwa mwenzako: Kujua kile ambacho ni muhimu sana kwa mpenzi wako kunaweza kusaidia sana kujenga nia njema na mazingira ya maelewano. Kwa upande mwingine, ni muhimu pia kwa mpenzi wako kutambua matakwa yako na wewe kuyaeleza kwa uwazi. Kutoa kila mara kwa mwingine kwa gharama ya mahitaji yako kutajenga tu chuki na hasira.

Kuwa na mazungumzo ya umuhimu

Mazungumzo ni mojawapo ya njia za msingi ambazo wanandoa wanaweza kuimarisha upendo wao. Ongea kuhusu hisia au matumaini au ndoto zako au mipango yako ya sasa au ya siku zijazo, au kile kinachokufanya uhisi kupendwa zaidi. Ikiwa mna mazungumzo hayo muhimu kwa uhusiano mtakuwa katika upendo zaidi.