Amini: Ni Wewe Lyrics na Maneno Ya Mapenzi

Posted by:

|

On:

|

Hapa kuna Ni Wewe Lyrics by Amini. Pia mwhisoni utapata jumbe za mapenzi kutokana kwa huu wimbo.

Amini: Ni Wewe Lyrics

Story yangu nilishakwambia, nilishawahi kuumizwa, ah!

Nikayumba na dunia, kwa penzi la dhuluma, ah!

Nashukuru wanipenda sana, karibu kwenye yangu dunia (yule)

Aliniacha kwenye jangwa (yule), sina hata maji (yule)

Nikajiita mkosaji (yule)

Si mara ya kwanza hii

Penzi letu lilipea imebaki story

Kila neno nililomwambia alikubaki kichwani, sasa

Ni wewe ul’onifanya naimba

Ni wewe sijakosea kupenda

Ni wewe unaenifanya nahema, aah

Ni wewe ul’onifanya naimba

Ni wewe sijakosea kupenda

Ni wewe unaenifanya nahema, aah

Nilipokufata nilikwambia

Hata mateso hutoyasikia

Bila kuwaza ukanipokea (uh, uh, uh, uh)

Si mpofu kupapasa baya na jema wavijua

Pasipo na njia uonyesha nia

Kwa maneno yoyo

Una malengo na mipango na viapo ndivyo

Nafurahi rohoni (lelo)

Sikumbuki zamani (lelo)

Umeibeba ramani (lelo)

Ya mapenzi duniani

Si mpofu kupapasa baya na jema wavijua

Ni wewe ul’onifanya naimba

Ni wewe sijakosea kupenda

Ni wewe unaenifanya nahema, aah

Ni wewe ul’onifanya naimba

Ni wewe sijakosea kupenda

Ni wewe unaenifanya nahema, aah

Ulinikuta kwenye jangwa, ukanipa maji

Mahututi sio wa kupumua, ukanipa uhai (aah)

Nikapata nguvu mpya, nikapooza makali (aah)

Maumivu uliyoyakuta yamekua asali

Aya ya-ya-ya, nafurahi rohoni (lelo)

Sikumbuki zamani (lelo)

Umeibeba ramani (lelo)

Ya mapenzi duniani

Si mpofu kupapasa baya na jema wavijua…

Ni wewe ul’onifanya naimba

Ni wewe sijakosea kupenda

Ni wewe unaenifanya nahema, aah

Ni wewe ul’onifanya naimba

Ni wewe sijakosea kupenda

Ni wewe unaenifanya nahema, aah

Ni wewe

Ni wewe

Ni wewe

Maneno ya mapenzi kutoka kwa “Amini- Ni Wewe Lyrics”

Hapa ni mistari ya mapenzi yenye imetumika kwa Ni Wewe lyrics, unaenza itumia kama SMS za kumtumia mpenziwe.

  • “Ni wewe ulionifanya naimba, ni wewe sijakosea kupenda, ni wewe unaenifanya nahema.”
  • “Ulinikuta kwenye jangwa, ukanipa maji, Mahututi sio wa kupumua, ukanipa uhai.”
  • “Nilipokufata nilikwambia, hata mateso hutoyasikia, bila kuwaza ukanipokea.”
  • “Si mpofu kupapasa baya na jema wavijua, Pasipo na njia uonyesha nia; Kwa maneno yoyo una malengo na mipango na viapo ndivyo.”
  • “Nafurahi rohoni sikumbuki zamani, umeibeba ramani ya mapenzi yetu.”