Hussein Machozi: Kwa Ajili Yako Lyrics na Maneno Matamu ya Mapenzi

Posted by:

|

On:

|

Hapa kuna Kwa Ajili Yako Lyrics by Hussein Machozi. Mwishoni utapata maneno matamu tumeunda kutoka kwa hizi lyrics yenye unaenza mtumia mpenzi wako.

Hussein Machozi: Kwa Ajili Yako Lyrics

Najua hiki ndo kipindi ukipendacho (Ukipendacho)

Najua sasa hivi upo karibu na radio (Radio)

Labda peke yako au na rafiki zako (Rafiki zako)

Naomba kidogo ongeza sauti ya radio

Nachukua nafasi kuongea nawe kwa wimbo (uh, uu, uuh)

Nimetunga special kwa ajili yako mrembo (uh, uu, uuh)

Mtangazaji kati ya wimbo usiweke jingle (uh, uu, uuh)

Nimetunga rasmii kwa mtu alie single (uh, aliye single uuh)

Kwa ajili yako naimba

Sauti hii sikia

Habari hii pokea

Zingatia mrembo, usipuuze mrembo

Zingatia mrembo, usipuuze mrembo

Zingatia aah aa, zingatia ahaa

(Ahaaaa)

Ndani yaroho yangu uko peke yako

Usihofu mamii hakuna mwenzako

Nimezaliwa mimi kwa ajili yako

Naahidi sitotupa penzi lako

Nimekupa nafasi kubwa ndani ya moyo (uh, uu, uuh)

Na ruksa tu niite baba watoto wako (uh, uu, uuh)

Kipingamizi hakuna juu yako (uh, uu, uuh)

Come closer nipunguze mapigo ya moyo (mapigo ya moyo)

Kwa ajili yako naimba

Sauti hii sikia

Habari hii pokea

Zingatia mrembo, usipuuze mrembo

Zingatia mrembo, usipuuze mrembo

Zingatia aah aa, zingatia ahaa

Moyo wangu unatamani sana

Mimi kuwa na wewe

Acha niseme hadharani

Kila mtu asikie

Moyo wangu unatamani sana

Mimi kuwa na wewe

Acha niseme hadharani

Kila mtu asikie

Asali ni tamu baby

Kwa anayefahamu

Ila ni chungu sana

Kwa asiyefahamu

Sogea karibu yangu

Tulia kabisa

Lala kifuani kwangu

Sinzia kabisa

Kwa ajili yako naimba

Sauti hii sikia

Habari hii pokea

Zingatia mrembo, usipuuze mrembo

Zingatia mrembo, usipuuze mrembo

Zingatia aahaa, zingatia ahaa

Wewee (zingatia)

Ahaaaa ahaaaa (zingatia)

Ahaaaa ahaaaa (zingatia)

Weweee (zingatia)

Ohoooo (zingatia)

Maneno matamu ya mapenzi kutoka kwa “Hussein Machozi Kwa Ajili Yako Lyrics”

  • Katika wimbo wa mapenzi, ninaimba wimbo uliotayarishwa kwa ajili yako tu, mrembo wangu. Uwepo wako ni kama wimbi la kutuliza, na ninatumai sauti yangu itafikia moyo wako.
  • Kama DJ wa hisia zako, ninamix nyimbo za mapenzi kwa ajili yako tu.
  • Katika upendo wetu, hatutaki kusumbuliwa. Nipe nafasi nipunguze mapigo ya moyo wako, na wimbo wetu wa mapenzi uwe wimbo wa safari yetu.
  • Ujumbe maalum kwako: Makini, mpenzi wangu, usidharau nguvu ya mapenzi yetu. Ujumbe huu sio maneno tu; ni tamko la hisia zangu kwako.
  • Upendo wetu ni utunzi wa kipekee, niwimbo ambao mimi na wewe tu tunaweza kucheza. Katika ukimya, acha mdundo wa mioyo yetu ulandane, na kwa umoja, tuunde hadithi ya upendo yenye upatanifu.
  • Acha sauti yangu iwe wimbo mzuri unaokaa moyoni mwako. Usiogope, mpenzi wangu; Nipo kwa ajili yako.