Mbosso: Haijakaa Sawa Lyrics na Maneno ya Nguvu kwa Mpenzi

Posted by:

|

On:

|

Hapa kuna “Haijakaa Sawa Lyrics” by Mbosso. Mwishoni utapata jumbe za kumfariji mpenzi na kumpa matumaini kutoka kwa huu wimbo.

Mbosso: Haijakaa Sawa Lyrics

Sasa unanuna nini?

Au unadhani hata mimi napenda

Nishazichoka na mimi

Mboga za majani kila siku mlenda

Siko juu siko chini

Niko nusu sadoo

Sio wa kumi si sabini

Ngoma ngumu bado

Kama ibada naswali sana

Usiku wa manane

Tena nafunga na Suna

Mambo bado bado mwana wane

Naona yanazidi kuguma

Nikirudi na hasira hasira (nizoee)

Mambo magumu bado bila bila (niombee)

Nikirudi na hasira hasira (nizoee)

Mambo magumu bado bila bila (niombee)

Halijakaa sawa

Nivumilie ipo siku tutapata

Halijakaa sawa

Shida na dhiki zitakwisha baby

Halijakaa sawa

Kuchana kope make up utapaka

Halijakaa sawa

Tutabadili mboga kuku kwa manyama

Chochea kuni kipenzi changu

Asubuhi tumbo likikuming’inya

Pokea kidogo changu

Tunywe chai na mkate wa kumimina

Akili ikichoka riziki nikikosa

Najua kwako nitajiliwaza

Kama makosa nivute chumbani

Kununa nuna unajilemaza

Ustahimilivu mnao wachache mno

Jua shida rafiki wa mbivu

Baada ya dhiki mavuno

Kila jema lina maumivu

Na kwenye waliopo tumo

Yarabi salama tupe tulivu

Penzi lisifike kikomo

Iyee eeh eeh

Nikirudi na hasira hasira (nizoee)

Mambo magumu bado bila bila (niombee)

Nikirudi na hasira hasira (nizoee)

Mambo magumu bado bila bila (niombee)

Halijakaa sawa

Nivumilie ipo siku tutapata

Halijakaa sawa

Shida na dhiki zitakwisha baby

Halijakaa sawa

Kuchana kope make up utapaka

Halijakaa sawa

Tutabadili mboga kuku kwa manyama

Maneno ya kumfariji mpenzi kutoka kwa “Mbosso: Haijakaa Sawa Lyrics”

  • Mambo bado mwana, naona yanazidi kuguma. Nikirudi na hasira nizoee, mambo magumu bado naomba uniombee.
  • Mambo bado sawa, nivumilie ipo siku tutapata na shida na dhiki zitakwisha baby.
  • Akili ikichoka riziki nikikosa najua kwako nitajiliwaza.
  • Jua shida rafiki wa mbivu, baada ya dhiki mavuno, kila jema lina maumivu.
  • Na kwenye waliopo tumo, Yarabi salama tupe tulivu, penzi lisifike kikomo.