MwanaFA: Asanteni Kwa Kuja Lyrics

Posted by:

|

On:

|

MwanaFA: Asanteni Kwa Kuja Lyrics

Choir master!

I’m in da building

Asanteni kwa kuja, thanks for coming

Coming, coming, coming, coming

Asanteni kwa kuja, thanks for coming

Coming, coming, coming, coming

Shombo nyingi zaidi ya soko la samaki

Ferry inangoja hata Beberu hanipati

Buheri wa afya, hofu juu yako

Merci beaucoup, njoo uongee na cousin yako

Naenda kazini wakati wanaenda vitandani

Sio salama. Sio salmini na silali ka vitani

Hakuna imani kwa ma-snitch mwana

Njoo na panga ukute shoka ka zamani zama

Bastola na glasi ya Vodka lazima kuwe na sadaka

Madeni lazima yalipwe hata mdaiwa asipotaka

Another day, another dollar (aa mi Mchaga mwingine)

Siku nyingine, hela nyingine

Sio kicheche mwingine

Asanteni kwa kuja, thanks for coming

Coming, coming, coming, coming

Asanteni kwa kuja, thanks for coming

Coming, coming, coming, coming

Here comes the beat, here comes the beast

Mother, I’m still the best

Ukiniona kimya imani na mshindo una-trot

Vita kwa vina money na auto in the bank

Kama ipo itafika tu, spika za nini kachaa

Mungu akitaka kukupa wala hakuandikii barua

We get money on the right things, and keep calm

Wenye kelele wote sio kings, kuwa na nidhamu

Tatizo la uongo ni kwamba milele haufiki mwisho

Ka kiporo utatudanganya na kesho

Malalamiko kibao ka mtoto wa kambo

Kuruka ruka haijawahi kuwa dawa ya ulimbo

Asanteni kwa kuja, thanks for coming

Coming, coming, coming, coming

Asanteni kwa kuja, thanks for coming

Coming, coming, coming, coming

Ilikuwa poa tu, ilikuwa love tu

Ilikuwa safi kabla mkwanja hujaleta makuu

Ilikuwa shega tu, ilikuwa peace tu

Ulikuwa mzuka ghafla mkwanja ukaleta upuuzi

Love iko mbali, chuki mwanzo mwisho bro

Hata mi ni hater ka hunipendi hivyo hivyo bro

Ulete ubwege na nikupende, mi ni Yesu?!

Hakuna shavu la pili, toa wembe nitoe kisu

Bado mshabiki mkubwa wa kazi ya Mungu

Ila kama nakuweza sikungoji nakupa kubwa wangu

Life yangu movie, na mi ndo director

Hata ukinielekeza sio kitu inakuwa extra

Asanteni kwa kuja, thanks for coming

Coming, coming, coming, coming

Asanteni kwa kuja, thanks for coming

Coming, coming, coming, coming