Roho yangu na ikuimbie lyrics

Posted by:

|

On:

|

Bwana Mungu Nashangaa Kabisa (How Great Thou Art) Swahili Lyrics

Roho yangu na ikuimbie lyrics

Bwana Mungu nashangaa kabisa,

Nikifikiri jinsi ulivyo,

Nyota, ngurumo, vitu vyote pia,

Viumbavyo kwa uwezo wako.

Roho yangu na ikuimbie,

Jinsi wewe ulivyo mkuu,

Roho yangu na ikuimbie,

Jinsi wewe ulivyo mkuu.

Nikitembea pote duniani,

Ndege huimba nawasikia,

Milima hupendeza macho sana,

Upepo nao nafurahia.

Roho yangu na ikuimbie,

Jinsi wewe ulivyo mkuu,

Roho yangu na ikuimbie,

Jinsi wewe ulivyo mkuu.

Nikikumbuka vile wewe Mungu,

Ulivyompeleka mwanao,

Afe azichukue dhambi zetu,

Kuyatambua ni vigumu mno.

Roho yangu na ikuimbie,

Jinsi wewe ulivyo mkuu,

Roho yangu na ikuimbie,

Jinsi wewe ulivyo mkuu.

Yesu Mwokozi atakaporudi,

Kunichukua kwenda mbinguni,

Nitaimba sifa zako milele,

Wote wajue jinsi ulivyo

Roho yangu na ikuimbie,

Jinsi wewe ulivyo mkuu,

Roho yangu na ikuimbie,

Jinsi wewe ulivyo mkuu.

Mungu ukubarikiwe