Rostam (Ft. Mr. Blue): Watani Wa Jadi Lyrics

Posted by:

|

On:

|

Watani wa jadi ni wimbo wa Rostam ft. Mr. Blue. Hapa ni lyrics za wimbo.

Watani Wa Jadi Lyrics

Ntakesha mkichoma ubani

Mpandishe Mashetani

Mkija kanzu tobo (waa yaa)

Mpira kwapani

Sisi mabingwa nyikani

Watoto wa jangwani

Labda aje simba wa yuda

Sio nyie simba wa mbugani

Yanga acheni usela

Usela mavi vueni jezi

Vaeni dear litawapendeza ilo vazi

Soka hamuwezi tuwape kibao cha mbuzi mkune nazi

Iko wazi hamna hadna hadhi mbele ya wekundu wa msimbazi

Hadhi gani eh eh, weku ndu gani

Kuku vikombe vya ligi nina vingi sina mpinzani

Aah wapi iyo iyo ligi kuu si rekodi yetu ya juu

Muungano tusker mtani jembe vikombe ka 52

Simba ya mafundi ni ile simba ya sandaland

Sio simba hii ya leo inayo fungwa mpaka na stendi

Nyinyi mlifungwa na mbao faie

Wachezaji mliokosa fikra, mkatoka mnachechemea

Ka demu aliye vunjwa bikra

Leao nimepita kariakoo

Kuna story imenikata stimu

Story gani, haji manara

Ndo mshika irizi wa timu

Mbona nyinyi mechi na ruvu mechi na ruvu

Mlifukia mbuzi golini

Kaka usitoe udhu, niache niende msikitini

Simba eeh, yanga eeh

Wote watani wajadi

Simba eeh, yanga eeh

Sisi watani wajadi, watani wajadi

Simba eeh, yanga eeh

Wote watani wajadi

Simba eeh, yanga eeh

Sisi watani wajadi, watani wajadi

Mi ni simba, kama kweli simba mikono juu

Mi ni yanga, kama kweli yanga mikono juu

Mi ni simba, kama kweli simba mikono juu

Mi ni yanga, kama kweli yanga mikono juu

Ila mpira ulikuwa zamani, kipindi cha lunyamila

Sekilojo chambua kilajalo tatu bila

Sasa unaletaje umwamba, mbele ya said kizota

Sande manara computer dimbani anaotesha ukoka

Enzi hizo winga ya kushoto, ana simana Thomas kipese

Cross anaipiga kwa ugoko, speed kana hiace ya mikese

Nyati nyatu George Masatu ??

Mzee wa kiminyio

Yebo yebo namba waliisoma

Mohamed Hussein machinga

Si tuna Joseph Kaniki

Vipi yanga ya canavaro

Sa pawasa unamuacha vipi ?

Una mkumbuka ally mayai, tembele alimwaga cheche

Mi namkumbuka nteze John uwanjani alikaanga kiepe

Wachezaji wenu bwana nini, kwa ndondo wanaudhi

Juzi nimemfuma mkude anacheza kombe kombe la mbuzi

Hata nyie mna dhiki hamuuziki alafu viburi

Mpaka mkawe ombaomba nakupitisha bakuli (tiwade buuuu)

Ee kid edea bendera ya simba tuna ipepea (semeni suuu)

Mkaozee segerea mme zoea kungoa viti Round hii haina fair

Unatokea tanga cha ajabu hauisapoti cost so

Uzalendo kwanza ndo maana unaitwaga mgosi

Niite roma kagere na coastal chama la nyumbani

Upo yanga wakati kwenu moro mtibwa turiani

Simba eeh, yanga eeh

Wote watani wajadi

Simba eeh, yanga eeh

Sisi watani wajadi, watani wajadi

Simba eeh, yanga eeh

Wote watani wajadi

Simba eeh, yanga eeh

Sisi watani wajadi, watani wajadi

Mi ni simba, kama kweli simba mikono juu

Mi ni yanga, kama kweli yanga mikono juu

Mi ni simba, kama kweli simba mikono juu

Mi ni yanga, kama kweli yanga mikono juu

Boss wenu kigeugeu mguu nje nguu ndani

Hakawii kupost twitter kuwa anabwaga hazarani

Boss wenu ninge muona mjanja ?

Haya tukote bongo twende club bingwa Afrika

Naija utaleta story zako za ac vita unakumbuka taifa nilicho Kufanya 2006

Unafufua makaburi, wakati hata nusu hukufika

Mamki tufunga mwaka huu nakunya dar mpaka moro

Mta ukalia na ndio mta jua kuwa ha mjui nyie utopolo

Bahata mumsajili nani bado mtakalia libolo Nini? Fc

Na mbona CCM na yanga kama zina rangi sawa

Aah aah, acha siasa usilete mambo yako ya ukawa

Duuh kweli yanga ana mimba

Basi nan simba kapakatwa, kwa mkapa kitawaka mfa vuja ka pakacha

Na round hii sahau kabisa kuhusu ubingwa

Timu gani haina duka mnauza jezi kama wamachinga

Kama mwanaume wa kweli rudi twewnde wote taifa

Simba jike we aka mkimbizi hauna jipya

Simba eeh, yanga eeh

Wote watani wajadi

Simba eeh, yanga eeh

Sisi watani wajadi, watani wajadi

Simba eeh, yanga eeh

Wote watani wajadi

Simba eeh, yanga eeh

Sisi watani wajadi, watani wajadi

Mi ni simba, kama kweli simba mikono juu

Mi ni yanga, kama kweli yanga mikono juu

Mi ni simba, kama kweli simba mikono juu

Mi ni yanga, kama kweli yanga mikono juu