Bwana ni mchungaji wangu lyrics na ujumbe muhimu

Posted by:

|

On:

|

Bwana Ni Mchungaji Wangu by Reuben Kigame and Jayne Yobera

Bwana ni mchungaji wangu lyrics

Bwana ni mchungaji wangu, sitapungukiwa kitu.

Hulaza kwenye majani mabichi, hunongoza kwa maji tulivu.

Hunihuisha nafsi yangu, hunioongoza kwa njia za haki.

Nipitapo bondeni mwa mauti, sitaogopa wewe u nami.

Siku zote za maisha yangu.

Hakika wema na fadhili zitanifuata mimi.

Nitakaa nyumbani mwa bwana, siku zote za maisha yangu.

Hakika wema na fadhili zitanifuata mimi.

Nitakaa nyumbani mwa bwana, siku zote za maisha yangu.

Gongo lako na fimbo yako vinanifiariji mimi.

Huandaa meza mbele yangu, machoni pa watesi wangu.

Hakika wema na fadhili zitanifuata mimi.

Nitakaa nyumbani mwa bwana, siku zote za maisha yangu.

Hakika wema na fadhili zitanifuata mimi.

Nitakaa nyumbani mwa bwana, siku zote za maisha yangu.

Hakika wema na fadhili zitanifuata mimi.

Nitakaa nyumbani mwa bwana, siku zote za maisha yangu.

Ujumbe wa nyimbo ya bwana ni mchungaji wangu

  • Mungu ndiye mchungaji anayetupatia mahitaji yetu yote. Wimbo unasema hatutapungukiwa na kitu maana Mungu ndiye mchungaji wetu.
  • Mungu hutuongoza kila mahali.” Hulaza kwenye majani mabichi, hunongoza kwa maji tulivu”, hii ni sitiari ya utunzaji wa Mungu kwa roho zetu.
  • Mungu huburudisha nafsi zetu na kutuongoza katika njia zilizo sawa. Hii ina maana kwamba Mungu hutupatia nguvu za kiroho na mwongozo.
  • Hata tukipita katika bonde la uvuli wa mauti, hatutaogopa, kwa maana Mungu yu pamoja nasi. Hii ni ahadi ya ulinzi wa Mungu na faraja wakati wa shida.
  • Wema na rehema za Mungu zitatufuata siku zote za maisha yetu. Hii ina maana kwamba upendo na huruma ya Mungu haitatuacha kamwe.
  • Tunaalikwa kukaa nyumbani mwa Bwana milele. Hii ni ahadi ya uzima wa milele pamoja na Mungu.